Viumbe Vipya Katika Kristo Yesu. || 10. KuTembea. || WaGalatia 5:14-26.
Pastor Joseph Muiruri
0:00 / 0:00
Viumbe Vipya Katika Kristo Yesu. || 10. KuTembea. || WaGalatia 5:14-26.
12 просмотров · 2 дн. назад
Pastor Joseph Muiruri
102 подписчика
12 просмотров · 2 дн. назад
1. WaGalatia 5:14-15. UTimilifu.
Torati yote inatimizwa katika Neno moja: Mpende Jirani yako kama nafsi yako. Ikiwa tunang’ata na kulaana sisi kwa sisi, tunapaswa kutambua tusije tumalizane sisi kwa sisi!
Funzo.
Bali ni wewe, mtu mwenzangu, Rafiki yangu, niliyejuana nawe sana: Zaburi 55:13.
Siwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo Bwana wake; lakini ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu: Yohana 15:15.
2. WaGalatia 5:16-18. KuTembea.
Kweli: Tunapotembea katika Roho Mtakatifu, hatutatimiza tamaa za mwili. Mwili hutenda kinyume na Roho Mtakatifu, na Roho Mtakatifu hutenda kinyume na mwili. Hivi viwili vinapingana, kiasi kwamba tunashindwa kufanya yale tunayotaka. Tukiongozwa na Roho Mtakatifu, hatuko chini ya Torati.
Funzo.
Ndipo Musa akasimama katika mlango wa marago, akasema, Mtu awaye yote aliye upande wa Bwana Mungu, na aje kwangu. Wana wa Lawi wote wakamkusanyikia: Kutoka 32:26.
Kama mtu akija kwangu naye hamchukii Baba yake, na Mama yake, na Mke wake, na Wanawe, na Ndugu zake waume na wake; naam, na hata Nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu: Luka 14:26
3. WaGalatia 5:19-21. MaTendo ya Mwili.
MaTendo ya mwili yako wazi: • ✓ a. UZinzi, • ✓ b. UAsherati, • ✓ UChafu, • ✓ d. UFisadi, • ✓ e. Ibada ya Sanamu, • ✓ f. UChawi, • ✓ g. Chuki, • ✓ h. UGomvi, • ✓ i. Wivu, • ✓ j. MiLipuko ya Hasira, • ✓ k. Tamaa za UBinafsi, • ✓ l. Fitina, • ✓ m. UZushi, • ✓ n. Husuda, • ✓ o. UUaji, • ✓ p. ULevi,
• ✓ q. Karamu za ULevi, • ✓ na mambo yanayofanana na hayo.
Haya yanatajwa kama yalivyotajwa hapo awali. Wale watendao mambo kama hayo hawataurithi UFalme wa Bwana Mungu.
Funzo.
Kumcha Bwana Mungu ni kuchukia uovu; Kiburi na majivuno, na njia mbovu, Na kinywa cha ukaidi pia nakichukia: Mithali 8:13
Mimi nimekuja ili niwe Nuru ya ulimwengu, ili kila mtu aniaminiye mimi asikae gizani: Yohana 12:46
4. WaGalatia 5:22-23. Tunda la Roho.
Tunda la Roho ni: • ✓ a. UPendo, • ✓ b. Furaha, • ✓ c. Amani, • ✓ d. UVumilivu, • ✓ e. Wema, • ✓ f. UTu Wema, • ✓ g. UAminifu, • ✓ h. UPole, • ✓ i. KujiZuia. Juu ya mambo kama hayo hakuna Torati.
Funzo.
Tazama, wapendezwa na kweli iliyo moyoni; Nawe utanijulisha hekima kwa siri: Zaburi 51:6.
Pilato akamwambia, Kweli ni nini? Naye akiisha kusema neno hilo akawatokea WaYahudi tena, akawaambia, Mimi sioni hatia yo yote kwake: Yohana 18:38.
5. WaGalatia 5:24-26. KuIshi.
Walio wa Kristo Yesu wameusulibisha Mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake. Tukiishi kwa Roho MTakatifu, na tuenende kwa Roho MTakatifu.
Tusijisifu bure, tukichokozana na kuhusudiana.
Funzo.
Sauli akamwonea Daudi wivu tangu siku ile: 1 Samweli 18:9.
Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano: Mathayo 15:19.
Wazo Kuu.
Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili: WaGalatia 5:16.
Tafakari.
Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha Mwili pamoja na mawazo yake mabaya na zake: WaGalatia 5:24.
Sala.
Tusijisifu bure, tukichokozana na kuhusudiana: WaGalatia 5:26.