Перейти к содержимому

KuFurahia Kuishi Katika Kristo Yesu8. KutoKuShtushwa: B.WaFilipi 4:14-23

Pastor Joseph Muiruri

0:00 / 0:00

KuFurahia Kuishi Katika Kristo Yesu8. KutoKuShtushwa: B.WaFilipi 4:14-23

32 просмотра · 2 мес. назад
Pastor Joseph Muiruri
102 подписчика
32 просмотра · 2 мес. назад
1. WaFilipi 4:14-16. Hongera. MTume Paulo anawapongeza kwa kufanya vyema kwa kushiriki katika dhiki yake. Anawakumbusha jinsi ilivyokuwa mwanzoni mwa kuhubiri Injili. Alipoondoka Makedonia, hakuna Kanisa lingine lililoshirikiana naye katika habari ya kutoa na kupokea. Ilikuwa wao peke yao. Hata alipokuwa Thesalonike, walimtumia msaada mara moja na tena kwa mahitaji yake. Funzo. Musa akaondoka na Yoshua, MTumishi wake, Musa akapanda Mlimani kwa Bwana Mungu: Kutoka 24:13. Na penye Msalaba wake Kristo Yesu walikuwa wamesimama mamaye, na umbu la mamaye, Mariamu wa Klopa, na Mariamu Magdalene. Basi Yesu alipomwona Mama yake, na yule MwanaFunzi aliyempenda amesimama karibu, alimwambia Mama yake, Mama, tazama, Mwanao! Yohana 19:25-26. 2. WaFilipi 4:17-18. KutoKuJitakia. MTume Paulo anasisitiza kwamba hatafuti zawadi. Anatafuta matunda yanayoongezeka katika hesabu yao. Anasema ana vyote na ameshiba, kwa kuwa amepokea kupitia Epafrodito kile walichomtumia. Anakieleza kuwa ni harufu nzuri yenye manukato, dhabihu inayokubalika na inayompendeza Bwana Mungu. Funzo. Dhabihu za Bwana Mungu ni roho iliyovunjika; Moyo uliovunjika na kupondeka, Ee Bwana Mungu, hutaudharau: Zaburi 51:17. Basi Yesu akamwambia Petro, Rudisha upanga alani mwake; Je! Kikombe alichonipa Baba, mimi nisikinywee? Yohana 18:11. 3. WaFilipi 4:19-20. Ahadi. MTume Paulo anatangaza kwamba Bwana Mungu wake atawajalia mahitaji yao yote kwa kadiri ya utajiri wake katika UTukufu ndani ya Kristo Yesu. Kwa Bwana Mungu wetu na Baba yetu kuwe UTukufu Milele na Milele. Amina!!! Funzo. Bwana Mungu atakulinda utokapo na uingiapo, angu sasa na hata Milele: Zaburi 121:8. UwaTakase kwa ile Kweli; Neno lako ndiyo Kweli: Yohana 17:17. 4. WaFilipi 4:21-23. Kuaga. MTume Paulo anatuma salamu kwa kila MTakatifu aliye katika Kristo Yesu. Pia anatuma salamu kutoka kwa Ndugu walio pamoja naye na WaTakatifu wote. Anataja hasa wale wa Nyumba ya Kaisari. Anawatakia Neema ya Bwana wetu Kristo Yesu iwe pamoja nao wote. Amina!!! Funzo. Iweni hodari na moyo wa ushujaa, msiogope wala msiwahofu; kwa maana Bwana Mungu, Bwana Mungu wako, yeye ndiye anayekwenda pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha: KumbuKumbu la Torati 31:6. Kwa kuwa Torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; Neema na Kweli zilikuja kwa mkono wa Kristo Yesu: Yohana 1:17. Wazo Kuu. Si kwamba nakitamani kile kipawa, bali nayatamani mazao yanayozidi kuwa mengi, katika Hesabu yenu: WaFilipi 4:17. Tafakari. Na Bwana Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika UTukufu, ndani ya Kristo Yesu: WaFilipi 4:19. Sala. Neema ya Bwana Yesu Kristo na iwe pamoja na roho zenu. Amina!!! WaFilipi 4:23.