Перейти к содержимому

Kuishi Kwa Furaha Katika Kristo Yesu. | Sifa: A.| WaFilipi 2:1-16.

Pastor Joseph Muiruri

0:00 / 0:00

Kuishi Kwa Furaha Katika Kristo Yesu. | Sifa: A.| WaFilipi 2:1-16.

87 просмотров · 3 месяца назад
Pastor Joseph Muiruri
102 подписчика
87 просмотров · 3 месяца назад
1. WaFilipi 2:1-4. Wito. Tumeitwa kuishi maisha yenye, i. faraja katika Kristo Yesu, ii. utulivu wa upendo, iii. ushirika wa Roho MTakatifu, iv. upendo wa dhati na v. rehema. Haya hufikisha utimilifu wa furaha tunapokuwa wenye: i. nia moja, ii. upendo mmoja, iii. umoja wa moyo na iv. kusudi moja. Hakuna nafasi ya tamaa ya ubinafsi wala majivuno. Tuendeshwe na unyenyekevu wa mawazo, kila mmoja akimhesabu mwenzake kuwa bora kumliko. Maslahi ya binafsi yanawekwa chini kwa kutanguliza maslahi ya wengine. Lesson. Mgeni hakulala njiani; Lakini nilimfungulia msafiri milango yangu: Ayubu 31:32. Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea: Luka 19:10. 2. WaFilipi 2:5-11. Kristo Yesu. ✓ i. WaFilipi 2:5-8. Unyenyekevu. Tunapaswa kuiruhusu nia yetu ifanane na ile ya Kristo Yesu. Yeye alikuwa katika hali ya UUngu, wala hakuona kuwa ni unyang'anyi kuwa sawa na Bwana Mungu. Hata hivyo, alijifanya Mwenyewe kuwa: i. asiye na sifa, ii. akachukua hali ya MTumishi MFungwa, iii. akaja katika mfano wa wanadamu, iv. akaonekana kama mwanadamu, v. akajinyenyekeza, vi. akawa mtiifu hata kufikia mauti, vii. naam, mauti ya Msalaba. Funzo. Tumesikia habari za kiburi cha Moabu; Ya kuwa ana kiburi kingi; Jeuri yake, na kiburi chake, na majivuno yake, Na jinsi alivyotakabari moyoni mwake: Yeremia 48:29. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu: Mathayo 11:29. ✓ ii. WaFilipi 2:9-11. KuTukuzwa. Kwa hivyo Bwana Mungu: i. alimtukuza sana na ii. akampa Jina lililo juu ya kila jina. Katika Jina la Kristo Yesu: i. Kila goti lipigwe, la walioko Mbinguni, Duniani, na chini ya Dunia. ii. Kila ulimi ukiri ya kuwa Kristo Yesu ni Bwana Mungu, kwa utukufu wa Bwana Mungu Baba. Funzo. Macho ya mwanadamu yaliyoinuka yatashushwa chini, na kiburi cha mwanadamu kitainamishwa, naye Bwana Mungu, Yeye peke Yake, atatukuzwa Siku hiyo: Isaya 2:11. Akasema, Tazama! Naona Mbingu zimefunguka, na Mwana wa Adamu amesimama mkono wa KuUme wa Bwana Mungu: MaTendo 7:56. 3. WaFilipi 2:12-15. Nuru. Utiifu wetu kielelezo daima unahitajika, sana zaidi: Tukitimiza Wokovu wetu wenyewe kwa hofu na tetemeko. Ni Bwana Mungu atendaye kazi ndani yetu, mawili kutaka na kutenda kwa mapenzi yake mema. Mambo yote yafanywe bila kunung'unika wala mabishano. Jinsi hiyo tutakuwa wasio na i. lawama na ii. hila, iii. watoto wa Bwana Mungu wasio na kosa. Tuko katikati ya kizazi kilichopotoka na kilichoharibika, ambamo tunapaswa kung'aa kama Nuru Duniani. Funzo. Nami nitakufanya wewe kuwa Taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza Jina lako; nawe uwe baraka: Mwanzo 12:2. Vivyo hivyo Nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye Mbinguni: Mathayo 5:16. 4. WaFilipi 2:16-18. KuFurahi. Tunapaswa kulishika kwa uthabiti Neno la Uzima. Hili litawafanya wale waliotuhubiria au kutufundisha wafurahi katika Siku ya Kristo Yesu. Itakuwa uthibitisho kwamba hawakukimbia bure wala hawakufanya kazi bure. Funzo. Akasema, Usimnyoshee kijana mkono wako, wala usimtendee neno; kwa maana sasa ninajua ya kuwa unamcha Bwana Mungu, iwapo hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee: Mwanzo 22:12. Kisha MFalme atawaambia wale walioko mkono wake wa KuUme, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini UFalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu: Mathayo 25:34. Wazo Kuu. Msitende neno lolote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake: WaFilipi 2:3. Tafakari. Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu: WaFilipi 2:5. Sala. Mpate kuwa wana wa Bwana Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaonekana kuwa MiAnga katika Ulimwengu: WaFilipi 2:15.