Перейти к содержимому

MGOMO WA MADEREVA WATIKISA MOSHI

Mwananchi Digital

0:00 / 0:00

MGOMO WA MADEREVA WATIKISA MOSHI

10 625 просмотров · 1 день назад
Mwananchi Digital
1,23 млн подписчиков
10 625 просмотров · 1 день назад
Madereva wa mabasi yaendayo mikoa mbalimbali nchini wamegoma kwa saa kadhaa katika Stendi Kuu ya Mabasi Moshi, mkoani Kilimanjaro, wakipinga utaratibu wa kukatwa alama za makosa ya barabarani baada ya kutozwa faini. Madereva hao wamesema utaratibu huo unawaweka katika adhabu mbili kwa kosa moja, wakieleza kuwa dereva anapotozwa faini ya Sh30,000 kwa kosa la barabarani, hapaswi pia kupunguziwa alama kwenye leseni yake kwa kosa hilo hilo. Hali hiyo ilisababisha baadhi ya mabasi kushindwa kuendelea na safari na kuwaacha abiria wakisubiri kituoni. Akizungumza na Mwananchi leo Septemba 29, 2026, dereva wa basi la Masalu, Shedrack Kaaya, amesema mfumo huo umeongeza mzigo kwa madereva na unaweza kuhatarisha ajira zao endapo alama kwenye leseni zao zitapungua kutokana na makosa wanayodai tayari wameyalipia kwa faini. Naye dereva wa mabasi ya Lim Safari, Emanuel Singine, amesema madereva wamekuwa wakibeba mzigo mkubwa wa adhabu, hata katika baadhi ya makosa yanayohusisha hali ya gari. Msimamizi wa Kituo cha Mabasi Moshi Mjini, Samwel Mlay, amesema mgomo huo umeathiri zaidi abiria waliokuwa tayari wamekata tiketi, baada ya baadhi ya madereva kuyapaki mabasi na kushindwa kuendelea na safari. Amesema viongozi wa Jeshi la Polisi, akiwamo Kamanda wa Polisi Mkoa na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, waliingilia kati na baadhi ya mabasi yaliyoathirika kupata madereva wengine na kuendelea na safari. Hata hivyo, Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani (RTO), Nassoro Sisiwaya, na Ofisa Mfawidhi wa LATRA Mkoa wa Kilimanjaro, Paul Nyelo, ambao walikuwepo katika eneo la stendi hiyo, hawakutaka kuzungumza na Mwananchi kuhusu mgomo huo na baadaye waliondoka katika eneo hilo.