Перейти к содержимому

KuFurahia Kuishi Katika Kristo Yesu. | 1. Kitendawili: A.| WaFilipi 1:1-18.

Pastor Joseph Muiruri

0:00 / 0:00

KuFurahia Kuishi Katika Kristo Yesu. | 1. Kitendawili: A.| WaFilipi 1:1-18.

50 просмотров · 4 мес. назад
Pastor Joseph Muiruri
102 подписчика
50 просмотров · 4 мес. назад
1. WaFilipi 1:1-2. Utangulizi. MTume Paulo na Timotheo wanajitambulisha kama WaTumishi WaFungwa wa Kristo Yesu. Wanawaandikia WaTakatifu wote walio katika Kristo Yesu huko Filipi, pamoja na MaAskofu na MaShemasi. Wanawatakia Neema na Amani zitokazo kwa Bwana Mungu Baba yetu na Bwana Kristo Yesu. Funzo. UFunuo aliouona Nabii Habakuki: Habakuki 1:1. Kwa maana mimi nami ni mtu niliyewekwa chini ya mamlaka, mwenye Askari chini yangu; nikimwambia huyu, Nenda, huenda; na huyu, Njoo, huja; na mtumwa wangu, Fanya hivi, hufanya: Luka 7:8 2. WaFilipi 1:3-8. Shukrani. MTume Paulo anaeleza shukrani kwa Bwana Mungu wake kila anapowakumbuka. Kanisa la WaFilipi liko katika kila Ombi lake kwa furaha. Hii ni kwa sababu ya ushirika wao katika Injili tangu siku ya kwanza. Ana ujasiri kwamba Bwana Mungu, ambaye ameanza kazi njema ndani yao, ataikamilisha hata siku ya Kristo Yesu. Anmtaja Bwana Mungu kuwa Shahidi wake: Anawaonea shauku sana wote kwa upendo wa Kristo Yesu. Funzo. Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwangu Mungu, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho: Yeremia 29:11. Kama vile Baba alivyonipenda mimi, nami nilivyowapenda ninyi, kaeni katika pendo langu: Yohana 15:9. 3. WaFilipi 1:9-11. Ombi. Sala ya Mtume kwa ajili yao: Kwamba ✓ • i. Pendo lao lizidi sana na tena sana katika maarifa na upambanuzi wote. ✓ • ii. Waelewe mambo yaliyo mema zaidi. ✓ • iii. Wabaki wanyofu na wasio laumika hata siku ya Kristo Yesu. ✓ • iv. Wajazwe matunda ya haki kupitia Kristo Yesu, kwa UTukufu na Sifa za Bwana Mungu. Funzo. Kila mmoja aliyeitwa kwa Jina langu, niliyemwumba kwa ajili ya UTukufu wangu; mimi nimemwumba, naam, mimi nimemfanya: Isaya 43:7. Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye Mbinguni: Mathayo 5:16. 4. WaFilipi 1:12-15. Kitendawili. MTume anawajulisha yaliyompata maishani mwake. Mambo yote yametokea kwa maendeleo ya Injili. Imejulikana kwa Walinzi wote wa Ikulu na wengine wote kwamba vifungo vyake viko katika Kristo Yesu. Hii imewafanya Ndugu wengi katika Bwana Mungu kuwa na ujasiri zaidi. Wamekuwa hodari zaidi kulinena Neno bila woga. Hata hivyo, wengine wanamhubiri Kristo Yesu kwa husuda na ugomvi, na wengine kwa nia njema. Funzo. WaKuu wake huhukumu ili wapate rushwa, na MaKuhani wake hufundisha ili wapate ijara, na MaNabii wake hubashiri ili wapate fedha; ila hata hivyo watamtegemea Bwana Mungu, na kusema, Je! Hayupo Bwana Mungu katikati yetu? Hapana neno baya lo lote litakalotufikia: Mika 3:11. Ole wenu WaAndishi na MaFarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnawafungia watu UFalme wa Mbinguni; ninyi wenyewe hamwingii, wala wanaoingia hamwaachi waingie: Mathayo 23:13. 5. WaFilipi 1:16-18. Injili. ✓ • i. WaFilipi 1:16-17. WaHubiri. Wapo wanaomhubiri Kristo Yesu kwa tamaa ya ubinafsi. Hawana unyofu, wakikusudia kuongeza mateso katika vifungo vya MTume Paulo. Wale wanaomhubiri Kristo Yesu kwa upendo, wanajua kwamba MTume amewekwa kwa ajili ya kuitetea Injili. Funzo. Maana ndivyo nilivyoagizwa kwa neno la Bwana Mungu, kusema, Usile chakula cho chote wala usinywe maji, wala usirudi kwa njia ile uliyoijia: 1 WaFalme 13:9. Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya UNabii kwa Jina lako, na kwa Jina lako kutoa pepo, na kwa Jina lako kufanya miujiza mingi? Mathayo 7:22. ✓ • ii. WaFilipi 1:18. Matokeo. Vipi basi? Katika njia mbili hizo, kuigiza au Kweli, Kristo Yesu anahubiriwa. Hivyo MTume Paulo anafurahia na naam, atafurahia. Funzo. Usikasirike kwa sababu ya watenda mabaya, Usiwahusudu wafanyao ubatili: Zaburi 37:1. Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu! Mathayo 7:23. Wazo Kuu. Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba Yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu: WaFilipi 1:6. Tafakari. Yadhuru nini? Lakini kwa njia zote, ikiwa ni kwa hila, au ikiwa ni kwa Kweli, Kristo Yesu anahubiriwa; na kwa hiyo nafurahi, naam, nami nitafurahi: WaFilipi 1:18 Sala: Na hii ndiyo dua yangu, kwamba pendo lenu lizidi kuwa jingi sana, katika hekima na ufahamu wote: WaFilipi 1:9