Перейти к содержимому

KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA MORNING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING / 06 OCTOBER 2026

KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH

0:00 / 0:00

KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA MORNING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING / 06 OCTOBER 2026

11 067 просмотров · Трансляция закончилась 23 ч назад
KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH
65,2 тыс. подписчиков
11 067 просмотров · Трансляция закончилась 23 ч назад
KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA MORNING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING / 06 OCTOBER 2026 SOMO : VISHINDE VIKWAZO VINAVYOKUSONGA ILI UWE NA MATOKEO IBADA YA MORNING GLORY Marko 5 : 22 - 34 22 Akaja mtu mmoja katika wakuu wa sinagogi, jina lake Yairo; hata alipomwona, akaanguka miguuni pake, 23 akimsihi sana, akisema, Binti yangu mdogo yu katika kufa; nakuomba uje, uweke mkono wako juu yake, apate kupona, na kuishi. 24 Akaenda pamoja naye; mkutano mkuu wakamfuata, wakimsonga-songa. 25 Na mwanamke mmoja mwenye kutoka damu muda wa miaka kumi na miwili, 26 na kuteswa mengi kwa mikono ya matabibu wengi, amegharimiwa vitu vyote alivyo navyo, kusimfae hata kidogo, bali hali yake ilizidi kuwa mbaya 27 aliposikia habari za Yesu, alipita katika mkutano kwa nyuma, akaligusa vazi lake; 28 maana alisema, Nikiyagusa mavazi yake tu, nitapona. 29 Mara chemchemi ya damu yake ikakauka, naye akafahamu mwilini mwake kwamba amepona msiba ule. 30 Mara Yesu, hali akifahamu nafsini mwake kwamba nguvu zimemtoka, akageuka kati ya mkutano, akasema, Ni nani aliyenigusa mavazi yangu? 31 Wanafunzi wake wakamwambia, Je! Wawaona makutano wanavyokusonga-songa, nawe wasema, Ni nani aliyenigusa? 32 Akatazama pande zote ili amwone yule aliyelitenda neno hilo. 33 Na yule mwanamke akaingiwa na hofu na kutetemeka, akijua lililompata, akaja akamwangukia, akamweleza kweli yote. 34 Akamwambia, Binti, imani yako imekuponya, enenda zako kwa amani, uwe mzima, usiwe na msiba wako tena. Luka 13 : 6 - 9 6 Akanena mfano huu; Mtu mmoja alikuwa na mtini umepandwa katika shamba lake la mizabibu; akaenda akitafuta matunda juu yake, asipate. 7 Akamwambia mtunzaji wa shamba la mizabibu, Tazama, miaka mitatu hii naja nikitafuta matunda juu ya mtini huu, nisipate kitu; uukate, mbona hata nchi unaiharibu? 8 Akajibu akamwambia, Bwana, uuache mwaka huu nao, hata niupalilie, niutilie samadi; 9 nao ukizaa matunda baadaye, vema! La, usipozaa, ndipo uukate. LENGO 1.Kukupa maarifa yatakayo kusaidia kuamsha na kutuumia uwezo wa ziada ulimo ndani yako ambao bado haujautumia. 2.Kutambua na kujua namna sahihi ya kushugulikia vikwazo vinavyo kuzuia kuwa na matokeo MAMBO YA KUTAFAKARI kama Bwana Yesu angekuwa hajasongwa je huyu mwanamke angelitumia njia aliyo itumia? kama huyu mwanamke asingetumia mbinu hii ya kujipenyeza je matokeo aliyoyapata angeliyapata? je! ni vikwazo gani vinavyo kusonga vinavyo kufanya usipate matokeo uliyo yatarajia? je! ni kwakiwango Gani umefanya jitihada kushinda vikwazo na kujipenyeza Ili uweze kupata unacho kihitaji? unadhani jitihada yako imetosha? Mhubiri: Mwl Ezekieli Malando Kwa maombi na ushauri : Mch. Kiongozi: Dkt. Eliona Kimaro Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053 Mch. Msaidizi: Anna Kuyonga Simu: +255 713 553 443 YouTube: Kijitonyama Lutheran church Barua Pepe : Kijitonyamalutheran@gmail.com