Перейти к содержимому

SEKTA YA BIMA INAVYOCHOCHEA USTAHIMILIVU, MAENDELEO NA UKUAJI WA UCHUMI WA TANZANIA

Tanzania Insurance Regulatory Authority [TIRA]

0:00 / 0:00

SEKTA YA BIMA INAVYOCHOCHEA USTAHIMILIVU, MAENDELEO NA UKUAJI WA UCHUMI WA TANZANIA

346 просмотров · 1 дн. назад
Tanzania Insurance Regulatory Authority [TIRA]
278 подписчиков
346 просмотров · 1 дн. назад
Sekta ya bima ni sehemu muhimu ya mfumo wa uchumi wa Taifa, ikiwa na mchango mkubwa katika kulinda maisha na mali, kudhibiti athari za hatari, kuimarisha uwekezaji na kuchochea shughuli za kiuchumi. Kupitia documentary hii, Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) inaangazia nafasi ya sekta ya bima katika kukuza uchumi wa Tanzania, mafanikio yaliyopatikana, maendeleo ya soko la bima, pamoja na fursa zilizopo za kuimarisha matumizi ya bima kwa wananchi, wafanyabiashara na taasisi mbalimbali. Makala hii inaonesha namna bima inavyosaidia kujenga ustahimilivu wa kifedha, kulinda shughuli za uzalishaji na biashara, na kuweka msingi imara wa ukuaji endelevu wa uchumi wa Taifa. Tazama, elewa na tambua mchango wa sekta ya bima katika kujenga uchumi imara na Tanzania yenye maendeleo endelevu. Kwa taarifa zaidi kuhusu sekta ya bima, elimu ya bima na shughuli za TIRA, tembelea na kufuatilia majukwaa rasmi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania.