VIJANA 40 WAPEWA MAHARI BURE NA KUFUNGISHWA NDOA - ZANZIBAR
ASAM Online TV
0:00 / 0:00
VIJANA 40 WAPEWA MAHARI BURE NA KUFUNGISHWA NDOA - ZANZIBAR
1 861 просмотр · 1 день назад
ASAM Online TV
22,1 тыс. подписчиков
1 861 просмотр · 1 день назад
Bi Maryam Ali Alyassi kutoka United Arab Emirates (UAE) amewalipia mahari vijana 40, baada ya kubaini changamoto zinazowakabili baadhi ya vijana katika kumudu gharama za mahari.
Msaada huo umefanya historia katika kijiji cha Paje, Mkoa wa Kusini Unguja, baada ya ndoa 40 kufungwa kwa wakati mmoja, hatua iliyowawezesha vijana hao kuanza safari mpya ya maisha ya ndoa.
Akizungumza katika hafla hiyo, Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Mahmoud Mussa Wadi, amewataka wanandoa hao kutunza ndoa zao, kuvumiliana na kuepuka vishawishi vinavyoweza kuvuruga familia zao.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Emirates Group amesema taasisi hiyo imeamua kuwasaidia vijana hao kutokana na changamoto wanazokabiliana nazo, huku akiahidi kuendelea kutoa msaada huo.
Kwa furaha kubwa, vijana hao wameeleza shukrani zao baada ya kutimiza hatua muhimu ya maisha, wakisema msaada huo umewapa fursa ya kuanza maisha ya ndoa bila mzigo wa gharama za mahari.
#AsamOnlineTV #AsamMediaGroup #Zanzibar #Paje #Ndoa #Mahari #Vijana #UAE #KusiniUnguja #IslamicMarriage