Njia Utakayoiendea (The Way You Should Go)- Zaburi 32:8
Binti Sayuni 50
0:00 / 0:00
Njia Utakayoiendea (The Way You Should Go)- Zaburi 32:8
181 просмотр · 1 месяц назад
Binti Sayuni 50
539 подписчиков
181 просмотр · 1 месяц назад
Katika maisha tunaweza kufika mahali ambapo hatujui njia ipi tuchukue, uamuzi gani tufanye, au Mungu anataka twende wapi. Lakini Mungu anaweza kutujilia na kutuonyesha njia tunayopaswa kuiendea.
Katika somo hili tunaangalia maisha ya Paulo, ambaye alikuwa na mwelekeo wake mwenyewe, lakini alipokutana na Yesu, mwelekeo wa maisha yake ulibadilishwa kabisa. Mungu hakumbadilisha tu Paulo, bali alimfunulia njia na kusudi alilokuwa amemwandalia. Katika Wagalatia 1, Paulo anaeleza jinsi wito na mwelekeo wake ulivyotoka kwa Mungu na si kwa mwanadamu.
📖 Zaburi 32:8
“Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; nitakushauri, jicho langu likikutazama.”
Huenda leo umesimama katika njia panda, hujui uelekee wapi. Ujumbe huu ni ukumbusho kwamba Mungu bado anaongoza, anafundisha na kuonyesha njia. Tunachohitaji ni kuwa tayari kumsikia na kufuata uongozi wake.
🙏🏽 Bwana akuonyeshe njia utakayoiendea na akupe neema ya kutembea ndani ya kusudi lake.
#MajiraYaKujiliwa #NjiaUtakayoiendea #Zaburi32 #Wagalatia1 #Paulo #UongoziWaMungu #KusudiLaMungu #KumsikiaMungu #NenoLaMungu #MafundishoYaBiblia #BintiSayuni50