MAKONDA KAMA KAWAIDA YAKE ATOA KAULI HII HAPA/RAIS ANATAKA KUIONA TANZANIA DUNIANI
Mwananchi Digital
0:00 / 0:00
MAKONDA KAMA KAWAIDA YAKE ATOA KAULI HII HAPA/RAIS ANATAKA KUIONA TANZANIA DUNIANI
5 636 просмотров · 1 день назад
Mwananchi Digital
1,23 млн подписчиков
5 636 просмотров · 1 день назад
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amesema michezo ni miongoni mwa sekta zinazoweza kuongeza uchumi wa Tanzania, akisisitiza umuhimu wa kuendelea kuiweka nchi kwenye ramani ya michezo barani Afrika.
Makonda amesema hayo leo, Oktoba 3, 2026, alipotembelea viwanja vya Makunganya, mkoani Morogoro ambako kunaendelea Mashindano ya Mbio za Magari ya African Rally Championship (ARC).
Akiwa katika viwanja hivyo, Waziri huyo amekagua maeneo mbalimbali yanayotumika katika mashindano hayo na kujionea namna yanavyoendelea, kabla ya kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa mashindano hayo kwa Taifa.
Amesema Serikali inaendelea kuweka mkazo katika michezo kutokana na mchango wake katika uchumi, huku akieleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, anataka kuiona Tanzania ikiwa kwenye ramani ya michezo barani Afrika.