Перейти к содержимому

MUHIMBILI YAFUNGUA NJIA MPYA KUOKOA MAMA, WATOTO TUMBONI

Mwananchi Digital

0:00 / 0:00

MUHIMBILI YAFUNGUA NJIA MPYA KUOKOA MAMA, WATOTO TUMBONI

1 598 просмотров · 3 дн. назад
Mwananchi Digital
1,23 млн подписчиков
1 598 просмотров · 3 дн. назад
Dar es Salaam. Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeanza hatua mpya ya kupambana na vifo vya mama na watoto kwa kuimarisha huduma ya Maternal-Fetal Medicine, kitengo maalumu kinachowahudumia wanawake wenye mimba hatarishi na kumfuatilia mtoto akiwa bado tumboni. Hatua hiyo imechukuliwa baada ya hospitali hiyo kubaini changamoto kubwa katika mfumo wa rufaa, ambapo mwaka jana ilipokea zaidi ya wanawake 2,500 kutoka hospitali nyingine kwa matatizo ya uzazi na kupoteza 109 kati yao. Katika hao, 104 walifika Muhimbili baada ya kujifungua wakiwa tayari wamepata matatizo, huku ni wanawake watano pekee waliofika kabla ya kujifungua. Kwa hiyo, hospitali hiyo sasa inalenga kubadili mfumo kutoka kusubiri mama afike akiwa katika hali mbaya na badala yake, kuwabaini mapema wanawake wenye mimba hatarishi, kuwafuatilia wakati wa ujauzito na kuchukua hatua kabla hali haijawa ya kutishia maisha. Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Dk Delilah Kimambo, amesema takwimu hizo zimeifanya hospitali hiyo kuangalia upya namna inavyoshirikiana na vituo vinavyowapeleka wagonjwa Muhimbili.