Перейти к содержимому

ALIYEFUFA NA KUTOWEKA AZUA TAHARUKI MPWAPWA

ITV Tanzania

0:00 / 0:00

ALIYEFUFA NA KUTOWEKA AZUA TAHARUKI MPWAPWA

10 350 просмотров · 14 ч назад
ITV Tanzania
1,37 млн подписчиков
10 350 просмотров · 14 ч назад
ALIYEFUFA NA KUTOWEKA AZUA TAHARUKI MPWAPWA #HABARI: Matukio ya kushtusha na kuzua sintofahamu yamegubika Kijiji cha Ng'hambi wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma, kufuatia kijana John Thomas Mahinyila (28), aliyeripotiwa kufa maji mkoani Morogoro Septemba 11 na kuzikwa Septemba 13 mwaka huu, kudaiwa kufufuka na kisha kutoweka tena. Familia ya marehemu imeeleza kuwa kabla ya tukio hilo, kijana huyo alikuwa akiwatokea na kuomba msaada, jambo lililowasukuma kufanya maombi ya pamoja yaliyosababisha ndugu yao huyo kuibuka ghafla akiwa hai, kabla ya kufungiwa chumbani na baadaye kutoweka kusikojulikana. Mama wa marehemu, Esther Chitongo, pamoja na kaka wa marehemu, Saimon Thomas, wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo lililowaacha wananchi na familia katika taharuki na simanzi kubwa. Wameeleza kuwa pamoja na kwamba simulizi hizo zinaweza kuonekana kama mazingaombwe au maigizo, kwao ni ukweli uliowaacha na maswali mengi yasiyo na majibu kuhusu hatima ya ndugu yao. Kwa upande wake, Serikali ya Kijiji cha Ng'hambi kupitia Mwenyekiti wake, Bwana William Samwel Mkuya, amekiri kuwepo kwa taharuki hiyo kijijini hapo ingawa serikali haiamini katika imani hizo za kishirikina na mazingaombwe. Mwenyekiti Mkuya amewataka wananchi kuendelea kuwa watulivu, kuacha kutawaliwa na hofu na kuruhusu vyombo vya dola pamoja na mamlaka husika kuchunguza kwa kina tukio hilo ili kubaini ukweli wa kinachoendelea. DHqGv/?mibextid=wwXIfr Powered by #MCHEZOSUPA ‎ ‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA: ‎- ‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M - Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV. ‎ ‎#ITVDigital #ITVUpdates ITVTanzania ‎Follow @itvtz @radioonetanzania ‎@capitaldigitaltanzania