WAKULIMA WAASWA KUTUNGA SHERIA NDOGO KULINDA MIUNDOMBINU YA UMWAGILIAJI
Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC)
0:00 / 0:00
WAKULIMA WAASWA KUTUNGA SHERIA NDOGO KULINDA MIUNDOMBINU YA UMWAGILIAJI
71 просмотр · 8 месяцев назад
Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC)
898 подписчиков
71 просмотр · 8 месяцев назад
📍 Monduli, Arusha.
Wakulima wa skimu za umwagiliaji wamehimizwa kutunga na kutekeleza sheria ndogo kupitia katiba za vyama vyao, ili kulinda miundombinu ya umwagiliaji dhidi ya uharibifu unaotokana na kuingizwa kwa mifugo mashambani.
Wito huo umetolewa kufuatia malalamiko ya mara kwa mara kutoka kwa wakulima kuhusu baadhi ya wafugaji wanaokiuka mipaka ya matumizi ya ardhi na kuingiza mifugo kwenye mashamba ya umwagiliaji, hali inayosababisha uharibifu mkubwa wa mifereji na miundombinu ya kupeleka maji mashambani.
Akizungumza katika mkutano wa wakulima wa Skimu ya Umwagiliaji Kabambe Majengo, wilayani Monduli mkoani Arusha, uliohusisha utiaji saini wa mkataba wa Uendeshaji, Usimamizi na Matunzo ya skimu chini ya mradi wa Mifumo Himilivu ya Chakula nchini (TFSRP–P4R).
Afisa Sheria wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Amina Mweta amesema ni muhimu sheria ndogo ziwepo na zitekelezwe kikamilifu ili kulinda uwekezaji mkubwa wa Serikali katika sekta ya umwagiliaji. Sheria hizi hazitapendelea upande wowote, bali zitaweka nidhamu kwa wakulima na wafugaji kuhusu matumizi sahihi ya miundombinu.”
Ameongeza kuwa sheria hizo zitasaidia kuhakikisha kila mshiriki katika kilimo na ufugaji anafuata taratibu bila kuvunja haki za wengine, hivyo kuongeza tija na kudumu kwa miundombinu hiyo kwa vizazi vijavyo.
Hata hivyo, baadhi ya wakulima wa skimu hiyo, akiwemo Mzee Issa Omary, wameishukuru Serikali kwa kuichagua skimu ya Kabambe Majengo kuwa miongoni mwa zitakazonufaika na Mradi wa Mifumo Himilivu ya Chakula (TFSRP–P4R), wakieleza kuwa wamekuwa wakikumbwa na changamoto ya muda mrefu ya uharibifu wa miundombinu kutokana na ukosefu wa matunzo ya kudumu.
Amesema kuwa, utiaji saini wa Mkataba wa Uendeshaji, Usimamizi na Matunzo wa skimu hiyo utasaidia wakulima kutambua wajibu wao katika kuilinda miundombinu iliyopo, ikiwemo kudhibiti uharibifu unaosababishwa na matumizi holela au ukosefu wa usimamizi madhubuti.
Skimu ya Umwagiliaji Kabambe Majengo, inayosimamiwa na Chama cha Wakulima wa Umwagiliaji Kabambe Majengo, iko katika kijiji cha Majengo na inahudumia jumla ya ekari 300 za kilimo cha Umwagiliaji. Kupitia skimu hii, wakulima 366.
Mazao yanayolimwa katika eneo hilo ni pamoja na viazi vitamu, migomba, mahindi, maharage na mboga mboga, ambayo yote huchangia katika kuboresha lishe, kipato na usalama wa chakula kwa wakulima na Taifa kwa ujumla.
Mwisho.