WAKULIMA JOBAJ WAASWA KULINDA CHANZO CHA MAJI
Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC)
0:00 / 0:00
WAKULIMA JOBAJ WAASWA KULINDA CHANZO CHA MAJI
28 просмотров · 8 месяцев назад
Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC)
897 подписчиков
28 просмотров · 8 месяцев назад
📍 Karatu, Arusha.
Wakulima skimu ya Umwagiliaji Jobaj iliyopo wilayani Karatu Mkoani Arusha wameaswa kuacha kulima kando ya vyanzo vya maji ili kuepusha vyanzo hivyo kutoweka na kusababisha uhaba wa maji kwa wakulima wa skimu hiyo na skimu jirani zinazotegemea chanzo hicho.
Wito huo umetolewa na Mhandisi Umwagiliaji Mkoa wa Arusha, William Simon katika mkutano na wakulima wa skimu hiyo.Amesema Serikali inafanya kila jitihada kuhakikisha mkulima anakuwa na Kilimo cha uhakika kwa kupata maji ya kutosha na kuleta tija.
Katika mkutano huo wa wakulima uliohusisha zoezi la utiaji saini mkataba wa Uendeshaji, Usimamizi na Matunzo ya skimu, utakaotekelezwa chini ya Mradi wa Mifumo Himilivu ya Chakula nchini (TFSRP-P4R), amesema Serikali kupitia wataalamu wake inaendelea na jitihada za kuhakikisha maji yanapatikana bila kuathiri chanzo cha maji ambacho ni kitovu cha wakulima wa eneo la bonde la Eyasi.
Ameongeza kuwa pamoja na jitihada zinazofanywa na Serikali kuhakikisha maji ya kutosha yanapatikana, wakulima wana wajibu wa kuhakikisha chanzo cha maji kinalindwa ili kuwa na Kilimo cha uhakika.
Aidha kwa upande wao wakulima wa skimu hiyo wameridhia kutia saini mkataba wa Uendeshaji, Usimazi na Matunzo ya skimu utakaotekelezwa kupitia mradi wa Mifumo Himilivu ya Chakula nchini (TFSRP-P4R), kwa kuwa mkataba huo utasaidia kukabiliana na changamoto zinazowakabili katika skimu hiyo, ikiwemo upungufu wa maji pamoja na miundombinu ya asili ambayo wamekuwa wakitumia kwa muda mrefu.
Akizungumza katika mkutano wa wakulima wa skimu hiyo, mkulima Hemedi Iddy na Faraji Philip wamesema mkataba huo utasaidia kudhibiti uharibifu wa miundombinu ya Umwagiliaji kwa kuwa mkataba huo unagusa pande zote mbili, watumiaji pamoja na waliopewa dhamana ya kusimamia miundombinu ya Umwagiliaji.
Skimu ya Jobaji ina ukubwa wa ekari 1,562.5, ambapo kwa sasa eneo linalomwagiliwa ni ekari 500 tu. Hata hivyo, kukamilika kwa ujenzi wa miundombinu ya Umwagiliaji kutapelekea kuongezeka kwa eneo linalomwagiliwa kufikia ekari 1,562.5, hivyo kuinua uzalishaji na uchumi wa wakulima wa kijiji cha Jobaji eneo linalonufaika na skimu hiyo.
Mazao yanayolimwa katika skimu hiyo ni pamoja na vitunguu, mahindi, mpunga na maharage. Kupitia mradi wa Mifumo Himilivu ya Chakula nchini (TFSRP–P4R), Tume inaendelea na ujenzi wa miundombinu ya kisasa pamoja na uchimbaji wa visima virefu ili kukabiliana na changamoto ya upotevu wa maji na mgawanyo usio sawa mashambani.