KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA MORNING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING | 25 AUGUST 2026
KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH
0:00 / 0:00
KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA MORNING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING | 25 AUGUST 2026
6 078 просмотров · Трансляция закончилась 2 недели назад
KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH
64 тыс. подписчиков
6 078 просмотров · Трансляция закончилась 2 недели назад
KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA MORNING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING | 25 AUGUST 2026
UJUMBE WA LEO: KUMSHINDA MCHAWI WA NJIA YAKO
Matendo 13 : 6 - 12
Hesabu 20 : 20 - 21
LENGO LA SOMO
Kukupa maarifa ya Kuomba ili kusughulikia Kila mchawi au kikwazo chochote kilichokaa kwenye njia yako kwa lengo la kukuzuia au kukuharibia mwendo
Matendo 13 : 6 - 12
6 Walipokwisha kupita katikati ya kisiwa chote mpaka Pafo, wakaona mtu mmoja, mchawi, nabii wa uongo, Myahudi jina lake Bar-Yesu;
7 mtu huyu alikuwa pamoja na liwali Sergio Paulo, mtu mwenye akili. Yeye liwali akawaita Barnaba na Sauli waje kwake, akataka kulisikia neno la Mungu.
8 Lakini Elima, yule mchawi (maana ndiyo tafsiri ya jina lake), akashindana nao, akitaka kumtia yule liwali moyo wa kuiacha ile imani.
9 Lakini Sauli, ambaye ndiye Paulo, akijaa Roho Mtakatifu, akamkazia macho,
10 akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyoka?
11 Basi, angalia, mkono wa Bwana u juu yako, nawe utakuwa kipofu, usilione jua kwa muda. Mara kiwi kikamwangukia na giza, akazunguka-zunguka na kumtafuta mtu wa kumshika mkono na kumwongoza.
12 Ndipo yule liwali, alipoyaona yaliyotendeka, akaamini, akiyastaajabia mafundisho ya Bwana.
NAMNA MCHAWI WA NJIA YAKO ANAVYOFANYA
i. Kuizuia sauti yako isisikike na isipate kibali masikioni mwa watu wanaotakiwa kukusikiliza.
Unatakiwa usikilizwe ili uonyeshe uwezo ulionao, upate nafasi
Unatakiwa usikilizwe ili utatue changamoto zako na wale watakao kusikiliza
Mwanzo 41 : 37 - 39
37 Neno hilo likawa jema machoni pa Farao, na machoni pa watumwa wake wote.
38 Farao akawaambia watumwa wake, Tupate wapi mtu kama huyu, mwenye roho ya Mungu ndani yake?
39 Farao akamwambia Yusufu, Kwa kuwa Mungu amekufahamisha hayo yote, hapana mwenye akili na hekima kama wewe.
ii. Kukufanya kukinai au kupuuzia Kila jambo la muhimu litakalo kupa hatua za kimaisha
(Anakufarakanisha na njia yako)
iii. Kupoteza umuhimu wako na umuhimu wa kile unachokifanya au kuinua mbadala wako au mbadala wa unachokifanya
Kutoka 7 : 10 - 12
10 Basi Musa na Haruni wakaingia kwa Farao, wakafanya vivyo kama Bwana alivyowaambia; Haruni akaibwaga fimbo yake chini mbele ya Farao, mbele ya watumishi wake, ikawa nyoka.
11 Ndipo Farao naye akawaita wenye akili na wachawi; na hao waganga wa Misri wakafanya vivyo kwa uganga wao.
12 Wakabwaga chini kila mtu fimbo yake, nazo zikawa nyoka; lakini fimbo ya Haruni ikazimeza fimbo zao.
iv. Kutangulia mbele kwenye kila mlango wako wa fursa unapofunguliwa
Danieli 4 : 5 - 9
5 Nikaota ndoto iliyonitia hofu; mawazo niliyokuwa nayo kitandani mwangu, na njozi za kichwa changu, zikanifadhaisha.
6 Basi nikatoa amri kwamba wenye hekima wote wa Babeli, waletwe mbele yangu, ili kunijulisha tafsiri ya ndoto ile.
7 Ndipo wakaingia waganga, na wachawi, na Wakaldayo, na wanajimu; nikawahadithia ile ndoto; wao wasiweze kunijulisha tafsiri yake.
8 Bali hatimaye Danieli akaingia mbele yangu, ambaye jina lake ni Belteshaza, kwa kufuata jina la mungu wangu; tena ndani yake inakaa roho ya miungu watakatifu; nikamhadithia ile ndoto, nikisema,
9 Ee Belteshaza, mkuu wa waganga, kwa sababu ninajua ya kuwa roho ya miungu watakatifu inakaa ndani yako, na ya kuwa hapana neno la siri likushindalo, niambie njozi za ndoto yangu niliyoiona, na tafsiri yake.
Mhubiri: Mwl. Ezekiel Malando
Kwa maombi na ushauri :
Mch. Kiongozi: Dkt. Eliona Kimaro
Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053
Mch. Msaidizi: Anna Kuyonga
Simu: +255 713 553 443
YouTube: Kijitonyama Lutheran church
Barua Pepe : Kijitonyamalutheran@gmail.com