Перейти к содержимому

Viumbe Vipya Katika Kristo Yesu. || 9. UHuru. || WaGalatia 5:1-13.

Pastor Joseph Muiruri

0:00 / 0:00

Viumbe Vipya Katika Kristo Yesu. || 9. UHuru. || WaGalatia 5:1-13.

27 просмотров · 9 дней назад
Pastor Joseph Muiruri
102 подписчика
27 просмотров · 9 дней назад
1. Wagalatia 5:1-4. MaShaka. WaGalatia wanahimizwa kusimama imara katika UHuru unaopatikana katika Kristo Yesu. Hawapaswi tena kunaswa katika kongwa la utumwa. MTume Paulo anasisitiza kwa nguvu kwamba wakichagua tohara, Kristo hatawafaidia chochote. Tendo hilo litaweka wajibu juu ya mtu kuitimiza Sheria yote, hivyo kuwa ametengwa na Kristo Yesu. Jaribio la kuhesabiwa haki kwa Sheria humfanya mtu kuwa ameanguka na kutoka katika Neema. Funzo. Bwana Mungu wa milele ndiye makazi yako, Na mikono ya milele i chini yako. Na mbele yako amemsukumia mbali adui; Akasema, Angamiza! Kumbukumbu la Torati 33:27. Nayo Nuru yang’aa gizani, wala giza halikuiweza: Yohana 1:5. 2. WaGalatia 5:5-6. Tumaini. Kwa njia ya Roho Mtakatifu tunangoja kwa hamu tumaini la haki kwa Imani. Katika Kristo Yesu, kutahiriwa au kutotahiriwa si jambo la maana. La muhimu ni Imani itendayo kazi kwa Upendo. Funzo. Siku ya hofu yangu nitakutumaini Wewe: Zaburi 56:3. Msiogope, enyi kundi dogo; kwa kuwa Baba yenu ameona vema kuwapa ule UFalme: Luka 12:32. 3. WaGalatia 5:7-10. KuKatishwaTamaa. Walikuwa wakati wote watu wa kuigwa. Swali: Ni nani aliyewazuia wasiitii Kweli? Hakika si Yeye aliyewaita. Chachu kidogo huchachusha donge lote. Hata hivyo, yote hayajapotea. Wanaweza kubaki thabiti katika Bwana Mungu. Yeyote anayewasumbua atahukumiwa. Funzo. Nena na MKutano, na kuwaambia, Ondokeni ninyi hapo karibu na maskani ya Kora, na Dathani, na Abiramu: Hesabu 16:24. Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio WaTeule: Mathayo 24:4. 4. WaGalatia 5:11-13. Huduma. MTume Paulo anasisitiza kwamba kama bado angehubiri tohara, asingeteswa. KiKwazo cha MSalaba kingekuwa kimekwisha. Tamaa yake ni kwamba wanaowasumbua wangekatwa waondolowe kabisa. WaGalatia wameitwa kwenye UHuru. UHuru huo haupaswi kutumiwa kuwa nafasi kwa ajili ya mwili, bali kwa UPendo kuhudumiana. Funzo. Mtumikieni Bwana Mungu kwa furaha; Njoni mbele zake kwa kuimba: Zaburi 100:2. Kristo Yesu akawaambia, Chakula changu ndicho hiki, niyatende MaPenzi yake aliyenipeleka, nikaimalize kazi yake: Yohana 4:34. Wazo Kuu. Katika ungwana huo Kristo Yesu alituandika Huru; kwa hiyo simameni, wala msinaswe tena chini ya kongwa la UTumwa: WaGalatia 5:1. Tafakari. Mmetengwa na Kristo Yesu, ninyi mtakao kuhesabiwa haki kwa Sheria; mmeanguka na kutoka katika hali ya Neema: WaGalatia 5:4. Sala. Maana ninyi, Ndugu, mliitwa mpate UHuru; lakini UHuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali tumikianeni kwa UPendo: WaGalatia 5:13.