Перейти к содержимому

DC MJINI AKAGUA MAENEO 9 KUBAINI HATARI

ASAM Online TV

0:00 / 0:00

DC MJINI AKAGUA MAENEO 9 KUBAINI HATARI

1 419 просмотров · 3 дня назад
ASAM Online TV
21,9 тыс. подписчиков
1 419 просмотров · 3 дня назад
Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Dkt. Said Haji Mrisho, amefanya ziara katika shehia tisa za Wilaya ya Mjini Unguja kwa lengo la kubaini maeneo yanayoweza kuathiriwa na mvua za El Niño na kuweka mikakati ya kudhibiti athari zinazoweza kujitokeza. Katika ziara hiyo, timu hiyo imebaini changamoto mbalimbali zinazoweza kuongeza madhara wakati wa mvua, ikiwemo mitaro michafu, mkusanyiko wa maji na uchafu pamoja na baadhi ya maeneo yenye changamoto za miundombinu ya barabara. Changamoto hizo zimeibua umuhimu wa kuchukua hatua mapema, hususan katika usafi wa mitaro na maeneo yanayoweza kuwa vituo vya mkusanyiko wa maji, ili kupunguza uwezekano wa athari wakati wa mvua. Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Mjini, Bi. Hasna Attai Masoud, amewataka wananchi kushiriki kikamilifu katika usafi wa mazingira, akieleza kuwa sehemu kubwa ya uchafuzi wa mazingira inasababishwa na shughuli za wananchi wenyewe. Amesema ushirikiano kati ya wananchi na Serikali ni muhimu katika kuhakikisha mitaro na maeneo ya makazi yanakuwa katika hali nzuri, hasa wakati wa maandalizi ya kukabiliana na mvua zinazotarajiwa. Miongoni mwa maeneo yaliyotembelewa ni Chumbuni, Mtumwajeni, Sebleni, Shauri Moyo, Mapinduzi, Saateni, Bulioni, Mlandege na Miyembeni. Ziara hiyo ni sehemu ya hatua za maandalizi ya kukabiliana na athari za mvua za El Niño, huku wananchi wakihimizwa kuchukua jukumu la kulinda usafi wa mazingira na kutoa taarifa kuhusu maeneo yenye changamoto. #ElNino #Mvua #WilayaYaMjini #Zanzibar #UsafiWaMazingira #Chumbuni #Mtumwajeni #Sebleni #ShauriMoyo #Saateni #Mlandege #AsamOnlineTV #ZanzibarNews #HabariZanzibar #TanzaniaNews #NewsUpdate #Trending #TikTokTanzania #InstagramTanzania #FYP #ForYou