MELI 201 ZATIA NANGA BANDARI YA MARUHUBI
ASAM Online TV
0:00 / 0:00
MELI 201 ZATIA NANGA BANDARI YA MARUHUBI
10 603 просмотра · 2 недели назад
ASAM Online TV
21,3 тыс. подписчиков
10 603 просмотра · 2 недели назад
Bandari ya Maruhubi imeendelea kupiga hatua katika shughuli zake, huku meli nyingi za mizigo zikiendelea kutumia bandari hiyo kushusha mizigo, hatua inayosaidia kupunguza msongamano wa meli za mizigo uliokuwa ukijitokeza katika Bandari ya Malindi.
Hayo yameelezwa na wasimamizi wa Bandari ya Maruhubi wakati Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA) ilipofanya ziara ya kutembelea na kukagua shughuli za bandari hiyo.
Bodi hiyo imeelezwa kuhusu maendeleo yanayoendelea katika Bandari ya Maruhubi pamoja na namna bandari hiyo inavyosaidia kurahisisha shughuli za usafirishaji na upokeaji wa mizigo.
Katika ziara hiyo, Bodi ya Wakurugenzi ya ZMA pia imekagua ujenzi wa Bandari ya Fumba, ambapo imeelezwa kuwa mradi huo umefikia hatua nzuri ya utekelezaji.
Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa Fumba Port, Ndg. Zamzam Hassan Mwinyi, amesema ushirikiano kati ya uongozi wa mradi na wananchi umeimarishwa, huku fidia zikiendelea kutolewa kwa wananchi ili kupisha shughuli za utekelezaji wa mradi huo.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar, amewataka watendaji wa mradi wa Bandari ya Fumba kuhakikisha wanailisha Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za mradi huo.
#AsamOnlineTV #Zanzibar #ZMA #Bandari #Maruhubi #BandariYaMaruhubi #FumbaPort #Fumba #Malindi #UsafiriBaharini #Mizigo #Uchumi #Miundombinu #Uwekezaji #ZanzibarNews #HabariZanzibar #TanzaniaNews #UtaliiZanzibar #TikTokTanzania #InstagramTanzania #Trending #FYP #ForYou #Viral #NewsUpdate