“UCHANGIAJI DAMU NI UWEKEZAJI” — TNCC YAUNGA MKONO ZOEZI LA AIDF LA KUOKOA MAISHA
TNCC BUSINESS TV
0:00 / 0:00
“UCHANGIAJI DAMU NI UWEKEZAJI” — TNCC YAUNGA MKONO ZOEZI LA AIDF LA KUOKOA MAISHA
66 просмотров · 1 месяц назад
TNCC BUSINESS TV
688 подписчиков
66 просмотров · 1 месяц назад
Katika kuunga mkono Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, sekta binafsi inaendelea kuonyesha kuwa mchango wake katika maendeleo ya Taifa hauishii kwenye uwekezaji na ukuaji wa biashara, bali pia katika kulinda rasilimali muhimu zaidi maisha ya watu.
Akizungumza katika “Zoezi la Uchangishaji Damu la Viongozi” (Executive Blood Drive) lililoandaliwa na AIDF, Afisa Mtendaji Mkuu wa Chemba ya Taifa ya Biashara (TNCC), Bw. Oscar Kissanga, alisema: “Sekta binafsi ni injini ya uchumi, lakini uchumi imara unahitaji jamii yenye afya bora.”
Alisisitiza kuwa damu salama inayopatikana kwa wakati ni muhimu katika kuokoa maisha ya akina mama wakati wa kujifungua, watoto, waathirika wa ajali na wagonjwa wanaohitaji matibabu ya haraka.
Kwa mujibu wa WHO, Tanzania ilikusanya unit 648,592 za damu mwaka 2024/2025, ikivuka lengo la unit 590,000. Hata hivyo, mahitaji ya damu salama yanaendelea kuifanya sekta na jamii kwa ujumla kuwa na wajibu wa kuchangia.
Kwa mtazamo wa Dira 2050, Taifa lenye uchumi shindani linahitaji watu wenye afya na nguvu kazi yenye tija. Hivyo, uchangiaji damu si tendo la huruma pekee, bali ni uwekezaji katika maisha, ustawi wa jamii na uchumi wa Taifa.