Перейти к содержимому

TARECU YATOA MAFUNZO NA UGAWAJI WA MIZANI YA KIDIGITALI KWA WAKULIMA WILAYA YA KILINDI

Kilindi Matukio

0:00 / 0:00

TARECU YATOA MAFUNZO NA UGAWAJI WA MIZANI YA KIDIGITALI KWA WAKULIMA WILAYA YA KILINDI

31 просмотр · 4 дня назад
Kilindi Matukio
26 подписчиков
31 просмотр · 4 дня назад
Wakulima na Wanachama wa Ushirika Wilaya ya Kilindi wamepatiwa mafunzo ya matumizi ya mizani ya kidigitali pamoja na zoezi la ugawaji wa mizani hiyo kwa Vyama vya Ushirika vilivyopo wilayani Kilindi. Mafunzo hayo yamefanyika katika Ukumbi Mkubwa wa Mikutano, Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi yakilenga kuwawezesha viongozi na wanachama wa Vyama vya Ushirika kupata uelewa wa matumizi sahihi ya mizani za kidigitali katika shughuli za uzalishaji na biashara za mazao. Mizani hiyo imepokelewa na Vyama vya Ushirika kutoka Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Tanga TARECU ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuimarisha uwazi, usahihi na ufanisi katika upimaji wa mazao, hususan wakati wa shughuli za ununuzi na uuzaji wa mazao ya wakulima. Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi unaendelea kusisitiza matumizi sahihi ya vifaa hivyo ili kuongeza uaminifu katika biashara za mazao na kulinda maslahi ya wakulima na Vyama vya Ushirika.