Перейти к содержимому

RC MAKAME AIPONGEZA MBOZI KUVUKA MALENGO MIAKA 3 MFULULIZO, KAHAWA YATAJWA CHANZO KIKUU CHA MAPATO.

MKOA WA SONGWE

0:00 / 0:00

RC MAKAME AIPONGEZA MBOZI KUVUKA MALENGO MIAKA 3 MFULULIZO, KAHAWA YATAJWA CHANZO KIKUU CHA MAPATO.

50 просмотров · 3 мес. назад
MKOA WA SONGWE
533 подписчика
50 просмотров · 3 мес. назад
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Jabiri Omari Makame, ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi kwa mafanikio makubwa katika ukusanyaji wa mapato ya ndani, akisema hatua hiyo inaonesha usimamizi mzuri wa rasilimali na uwajibikaji wa viongozi pamoja na watendaji wa halmashauri hiyo. Mhe. Makame amesema Halmashauri ya Mbozi imeendelea kuimarisha makusanyo ya mapato kutoka mwaka wa fedha 2022/2023 hadi 2025/2026. Ameeleza kuwa mwaka 2022/2023 halmashauri ilikuwa imekadiria kukusanya shilingi bilioni 3.35 lakini ilifanikiwa kukusanya shilingi bilioni 5.5. Aidha, amesema katika mwaka wa fedha 2025/2026, halmashauri ilikuwa imejiwekea lengo la kukusanya shilingi bilioni 6.8, lakini hadi sasa imefanikiwa kukusanya shilingi bilioni 12.8, sawa na asilimia 115.35 ya lengo, jambo alilolitaja kuwa ni mafanikio makubwa yanayostahili pongezi. Kutokana na mafanikio hayo, Mkuu huyo wa Mkoa aliwapongeza Mwenyekiti wa Halmashauri, Baraza la Madiwani, Mkurugenzi wa Halmashauri, timu ya menejimenti, Mkuu wa Wilaya pamoja na vyombo vya ulinzi, usalama na viongozi wa Chama kwa ushirikiano wao uliochangia kufikiwa kwa matokeo hayo. Hata hivyo, Mhe. Makame alitoa tahadhari kuhusu utegemezi mkubwa wa mapato ya halmashauri kwenye zao la kahawa. Alieleza kuwa takwimu zinaonesha asilimia 41.34 ya mapato ya ndani, sawa na zaidi ya shilingi bilioni 5.5, yanatokana na zao hilo pekee. Alibainisha kuwa vyanzo vingine vikubwa vya mapato ni ushuru wa mazao ya mahindi unaochangia takribani shilingi bilioni 2, uuzaji wa viwanja unaochangia asilimia 8.8, pamoja na ushuru wa nyumba unaochangia asilimia 4 ya mapato ya halmashauri. Mhe. Makame alisisitiza umuhimu wa kuendelea kubuni na kuimarisha vyanzo vingine vya mapato ili kupunguza utegemezi wa zao moja na kuhakikisha mapato ya halmashauri yanaendelea kuwa imara na endelevu.