CHANGAMOTO YA MAJI YA ZIWA RUKWA KUVAMIA MAKAZI YA WANANCHI KAMSAMBA, RC KUNENGE ATOA KAULI
MKOA WA SONGWE
0:00 / 0:00
CHANGAMOTO YA MAJI YA ZIWA RUKWA KUVAMIA MAKAZI YA WANANCHI KAMSAMBA, RC KUNENGE ATOA KAULI
64 просмотра · 2 недели назад
MKOA WA SONGWE
533 подписчика
64 просмотра · 2 недели назад
CHANGAMOTO YA MAJI YA ZIWA RUKWA KUVAMIA MAKAZI YA WANANCHI KAMSAMBA, RC KUNENGE ATOA KAULI
MOMBA, SONGWE: Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Abubakar Mussa Kunenge, ameahidi kuchukua hatua za haraka katika kushughulikia changamoto na adha inayowakabili wananchi wanaoishi kandokando ya Ziwa Rukwa, kutokana na maji ya ziwa hilo kuvamia na kuharibu makazi yao.
Mhe. Kunenge amesema kuwa changamoto hiyo imekuwa ikiwapa adha wananchi, hususan wakazi wa Tarafa ya Kamsamba, Kata ya Ivuna, katika Wilaya ya Momba, ambao makazi yao yamekuwa yakiathiriwa na maji ya Ziwa Rukwa.
Amesema Serikali italifanyia kazi suala hilo kwa haraka ili kutafuta ufumbuzi wa changamoto hiyo na kupunguza athari zinazowakabili wananchi wanaoishi katika maeneo hayo.
Mkuu huyo wa Mkoa ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kukagua na kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri ya Momba