Перейти к содержимому

HAWA WAMESUSIA UZINDUZI WA BARAZA VYAMA VINGINE VYA SHIRIKI/MUTUNGI HATUWEZI KUWALAZIMISHA

Mwananchi Digital

0:00 / 0:00

HAWA WAMESUSIA UZINDUZI WA BARAZA VYAMA VINGINE VYA SHIRIKI/MUTUNGI HATUWEZI KUWALAZIMISHA

3 488 просмотров · 1 день назад
Mwananchi Digital
1,23 млн подписчиков
3 488 просмотров · 1 день назад
Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi amesema vyama 18 vya siasa vimeshiriki katika uzinduzi wa uongozi mpya na nembo ya Baraza la Vyama vya Siasa, huku chama kimoja kikikosekana katika shughuli hiyo. Jaji Mutungi amesema ushiriki huo unaonyesha umuhimu wa Baraza hilo kama jukwaa la kukutanisha vyama vyenye itikadi na mitazamo tofauti kwa ajili ya kusikilizana, kujadiliana na kutafuta suluhu katika masuala yenye maslahi ya taifa. Amesema pamoja na ushindani unaojitokeza wakati wa uchaguzi wa viongozi wa Baraza, baada ya uchaguzi kukamilika wajumbe wanapaswa kurejea katika ari ya ushirikiano na mshikamano, huku maslahi ya taifa yakiwekwa mbele ya tofauti za kisiasa na kiitikadi. “Vyama vina itikadi zao tofauti, lakini tunapokuja kwenye masuala ya kitaifa tunaweza kukaa pamoja, tukazungumza hata pale tunapopishana, lakini tukatafuta mwafaka wa kuibuka na hoja ambazo ni za kitaifa zaidi,” amesema Jaji Mutungi. #Video