Перейти к содержимому

Harufu Kali na Nzi Wawatesa Wakazi wa Kiteje kwa Miaka Miwili

Dusted Lens News-Kenya

0:00 / 0:00

Harufu Kali na Nzi Wawatesa Wakazi wa Kiteje kwa Miaka Miwili

768 просмотров · 3 месяца назад
Dusted Lens News-Kenya
209 подписчиков
768 просмотров · 3 месяца назад
Wakazi wa Kijiji cha Kiteje katika Kaunti ya Kwale wameelezea hofu ya kuzuka kwa magonjwa ya mlipuko, yakiwemo kipindupindu na matatizo mengine ya afya, kutokana na utupaji holela wa kinyesi cha kuku kutoka kwa shamba la mfanyabiashara mmoja eneo hilo. Wakazi hao wanasema wamekuwa wakikumbana na hali hiyo kwa takriban miaka miwili, jambo ambalo limeathiri maisha yao ya kila siku na kuwanyima utulivu kutokana na harufu kali, wingi wa nzi na hofu ya magonjwa yanayotokana na uchafu huo. Sasa wanaitaka serikali na idara husika kuingilia kati haraka ili kupata suluhisho la kudumu, wakidai kuwa malalamiko yao ya awali hayajazaa matunda.