RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN ATEKELEZA AHADI YA GARI KWA SHULE YA WASICHANA BEATRICE SHELUKINDO
Kilindi Matukio
0:00 / 0:00
RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN ATEKELEZA AHADI YA GARI KWA SHULE YA WASICHANA BEATRICE SHELUKINDO
454 просмотра · 1 месяц назад
Kilindi Matukio
24 подписчика
454 просмотра · 1 месяц назад
Tarehe 18 Julai 2026 Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Mhe. Hashim Mgandilwa amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika hafla ya kukabidhi gari lililotolewa na Rais kwa Shule ya Wasichana Beatrice Shelukindo
Katika hafla hiyo, Mhe. Mgandilwa alimkabidhi rasmi gari hilo Mkuu wa Shule, Bi. Selestina Gasper Kavishe mbele ya viongozi mbalimbali, Bodi ya Shule, walimu, wanafunzi na wananchi.
Aidha kwa Upande wa Wanafunzi wamempongeza na Kutoa shukrani za dhati kwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza ahadi aliyowapa, wakieleza kuwa msaada huo utaimarisha shughuli za uendeshaji wa shule na kuchochea mazingira bora ya kujifunzia. Shukrani pia zilitolewa kwa Bodi ya Shule na wadau wote walioendelea kushirikiana katika maendeleo ya elimu.
Serikali inaendelea kuweka mazingira wezeshi ya kuinua elimu ya watoto wa kike na kuhakikisha taasisi za elimu zinapata huduma na miundombinu inayohitajika kwa maendeleo ya taifa.