SALAMU ZA EID ZASOGEZA MUSTAKABAL WA ZANZIBAR
ZANZIBAR YETU
0:00 / 0:00
SALAMU ZA EID ZASOGEZA MUSTAKABAL WA ZANZIBAR
9 317 просмотров · 5 месяцев назад
ZANZIBAR YETU
10,3 тыс. подписчиков
9 317 просмотров · 5 месяцев назад
Rais wa Zanzibar Hussein Mwinyi, amewanasihi waumini wa dini ya Kiislamu na jamii kwa ujumla kuendeleza utaratibu mzuri wa kuwasaidia na kuwahurumia watu wasio na uwezo kwa kuzingatia mahitaji yao maalumu.
Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 21 Machi 2026, katika Baraza la Eid el-Fitri lililofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Polisi, Ziwani, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Alisema ili kuwa na jamii yenye ustawi bora, ni vema utaratibu huo ukaendelezwa kwani kwa kiasi kikubwa umewasaidia watu wa makundi maalumu, wakiwemo mayatima, wajane na mafakiri, kupata futari na kutekeleza ibada ya funga kikamilifu.
Waumini wa dini ya Kiislamu wana wajibu mkubwa wa kutekeleza na kuendeleza mambo yote ya kheri yaliyokuwa yakifanyika katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, ikiwemo kumcha Mwenyezi Mungu kwa bidii, kwani yanaongeza upendo, umoja na mshikamano.
Ameeleza kuwa kufanyika kwa mashindano ya Tahfidh Qur’an na Tajweed ya kitaifa na kimataifa, pamoja na darsa mbalimbali zilizofanyika katika misikiti mijini na vijijini, kumesaidia waumini kutekeleza ibada kwa usahihi na pia kunachangia kwa kiasi kikubwa kuwarithisha vijana na watoto kuishi kwa kuzingatia maadili mema na kuwa na hofu ya Mwenyezi Mungu.
Akizungumzia Sikukuu ya Eid el-Fitri, amelitaka Jeshi la Polisi kusimamia na kuhakikisha usalama na amani vinaimarishwa katika viwanja vya sikukuu, pamoja na kusisitiza usimamizi madhubuti wa sheria za usalama barabarani ili kuhakikisha wananchi wanasherehekea sikukuu kwa amani na utulivu.
Kwa upande wa suala la Hijjah, amesema Serikali itaendelea kushirikiana na taasisi zinazosafirisha mahujaji kupitia Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana ili kuhakikisha Waislamu wanaokwenda kutekeleza ibada ya Hijjah wanaongezeka. Aidha, ameeleza kuwa Serikali inaendelea na utaratibu wa kukamilisha kuanzishwa kwa mfuko maalum wa Hijjah.
Baraza la Eid limehudhuriwa na Mke wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Mama Mariam Mwinyi, viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, akiwemo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein, Makamu wa Pili wa Rais Mstaafu, Balozi Seif Ali Iddi, Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Saleh Omar Kaabi, Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mhe. Zuberi Ali Maulid, pamoja na viongozi wa dini, masheikh na waumini mbalimbali.
Awali Mwinyi alijumuika na waumini wa dini ya Kiislamu kusali Sala ya Eid el-Fitri kitaifa katika Msikiti wa Jamiu Zanzibar, Kiembe Samaki, Mkoa wa Mjini Magharibi, na baadaye kuelekea Ikulu kwa ajili ya kutoa mkono wa Eid kwa mamia ya watoto na wananchi, wakiwemo wajane na wenye mahitaji maalumu, na kuwatakia heri na baraka katika kusherehekea Sikukuu ya Eid el-Fitri.