Перейти к содержимому

TFF YAINGILIA KATI UCHAGUZI SIMBA, IKIPIGA MKWARA MZITO, YAFAFANUA WALICHOKUBALIANA MANGUNGU, MAGORI

Mwananchi Digital

0:00 / 0:00

TFF YAINGILIA KATI UCHAGUZI SIMBA, IKIPIGA MKWARA MZITO, YAFAFANUA WALICHOKUBALIANA MANGUNGU, MAGORI

35 522 просмотра · 10 ч назад
Mwananchi Digital
1,23 млн подписчиков
35 522 просмотра · 10 ч назад
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeamua kusimamia moja kwa moja mchakato wa uchaguzi wa Simba SC unaotarajiwa kufanyika Januari 3, 2027 baada ya kubaini mapungufu katika ratiba iliyotolewa awali na klabu hiyo, hatua inayolenga kuhakikisha zoezi hilo linafanyika kwa kuzingatia katiba, kanuni na taratibu. Akizungumza na Wanahabari leo Novemba 1, 2026 jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Wakili Kiomoni Kibamba, amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya kamati yake kupokea malalamiko kuhusu utaratibu uliotumiwa na Bodi ya Wakurugenzi ya Simba Sports Club Company katika kuandaa uchaguzi. Amesema kamati ilipokea barua mbili kupitia Ofisi ya Katibu Mkuu wa TFF. Barua ya kwanza ilitoa taarifa ya kuanza kwa mchakato wa uchaguzi wa Simba, huku nyingine ikiwa na malalamiko kuhusu utaratibu uliotumiwa na bodi hiyo. Kutokana na hali hiyo, kamati iliamua kuwasikiliza wahusika wa pande zote kabla ya kutoa maelekezo kuhusu namna uchaguzi utakavyoendeshwa. Kibamba amesema walifanya mazungumzo na wawakilishi wa pande mbili, akiwamo Crescentius Magori aliyewakilisha upande wa mwekezaji na Murtaza Mangungu kwa upande wa wanachama, hivyo wamekubaliana uchaguzi utafanyika kwa ratiba ilivyopangwa awali lakini ratiba ya matukio ndio itabadilika. Baada ya mazungumzo hayo, kamati ilisisitiza kuwa uchaguzi wa viongozi wa upande wa wanachama na mwekezaji lazima ukamilike kabla ya muda wao wa uongozi kumalizika Januari 29, 2027. Viongozi hao walichaguliwa Januari 29, 2023, kwa kipindi cha miaka minne kwa mujibu wa Katiba ya Simba na kanuni za TFF. Hata hivyo, amesema kamati imebaini mapungufu mawili katika ratiba ya uchaguzi iliyokuwa imetolewa na kamati iliyoundwa na Bodi ya Simba. Amefafanua kuwa ratiba hiyo haikuweka utaratibu wa rufaa kwa wagombea ambao hawataridhishwa na maamuzi ya uteuzi, pamoja na masuala ya maadili ambayo ni sehemu muhimu ya mchakato wa uchaguzi. ✍️ @solojr 🎥 @nyembe_b46