Перейти к содержимому

POLISI HAI YATOA ELIMU YA UHALIFU NA DAWA ZA KULEVYA KWA WANAFUNZI WA LYAMUNGO SEKONDARI.

HENRY KETO

0:00 / 0:00

POLISI HAI YATOA ELIMU YA UHALIFU NA DAWA ZA KULEVYA KWA WANAFUNZI WA LYAMUNGO SEKONDARI.

107 просмотров · 5 дней назад
HENRY KETO
19 подписчиков
107 просмотров · 5 дней назад
‎‎Jeshi la Polisi Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, kupitia Kitengo cha Polisi Jamii, limetoa elimu kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Lyamungo kuhusu madhara ya vitendo vya kihalifu, matumizi ya dawa za kulevya pamoja na umuhimu wa kuzingatia nidhamu shuleni. ‎ ‎Elimu hiyo imetolewa Agosti 24, 2026, katika Shule ya Sekondari Lyamungo, ambapo Afisa Mnadhimu wa Polisi Wilaya ya Hai, OCD SSP Suzan Kidiku, amewataka wanafunzi kuachana na vitendo vyote vya kihalifu na matumizi ya dawa za kulevya, akisisitiza umuhimu wa kulinda mustakabali wao. ‎ ‎SSP Suzan Kidiku amesema matumizi ya dawa za kulevya pamoja na utovu wa nidhamu vinaweza kuathiri kwa kiasi kikubwa ufaulu wa mwanafunzi na uwezo wake wa kujifunza. Aidha, ameeleza kuwa baadhi ya vitendo hivyo vinaweza kuwa kikwazo kwa vijana kupata fursa mbalimbali za ajira na maendeleo baada ya kumaliza masomo. ‎ ‎Kwa upande wake, Mkuu wa Polisi Jamii Wilaya ya Hai, SP Elishafra, amesema ziara hiyo imelenga kutoa elimu na hamasa kwa wanafunzi kuhusu umuhimu wa kuwa na nidhamu, kujiepusha na uhalifu na kuzingatia masomo yao. ‎ ‎SP Elishafra amesema Shule ya Sekondari Lyamungo ina historia ya kutoa viongozi mbalimbali mashuhuri, akiwataja Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania, Frederick Sumaye, pamoja na viongozi wengine. ‎ ‎Ametoa wito kwa wanafunzi hao kutumia fursa waliyonayo ya kupata elimu kwa kujituma katika masomo, kuwa na nidhamu na kuepuka makundi au vitendo vinavyoweza kuharibu maisha yao, ili waweze kujenga uwezo na kufikia ndoto zao hapo baadaye. ‎ ‎#PolisiJamii #Hai #Kilimanjaro #Elimu #DawaZaKulevya #Uhalifu #Nidhamu #Lyamungo