Darsa: حُقُوْقُ الزَّوْجَةِ عَلَى زَوْجِهَا 🔴LIVE|DARSA Haki za Mke juu ya Mume (III)Ust. Abu Raifah
Darsa na Mihadhara
0:00 / 0:00
Darsa: حُقُوْقُ الزَّوْجَةِ عَلَى زَوْجِهَا 🔴LIVE|DARSA Haki za Mke juu ya Mume (III)Ust. Abu Raifah
43 просмотра · Трансляция закончилась 12 дней назад
Darsa na Mihadhara
863 подписчика
43 просмотра · Трансляция закончилась 12 дней назад
Darsa ilifanyika Rabi'ul Awwal 17, 1448 H Jumapili Agosti 30, 2026
SEHEMU YA TATU
Haki za Mke juu ya Mumewe حُقُوْقُ الزَّوْجَةِ عَلَى زَوْجِهَا
Kama ambayo Sharia imewajibisha imelazimisha kwa mke kutimiza fungu la haki kwa mumewe, kadhalika Sharia imempa imemuwekea mke haki zinazohifadhi Dini yake na hadhi yake.
:قال تعالى
﴾وَلَهُنَّ مِثْلُ الَّذِي عَلَيْهِنَّ بِالْمَعْرُوفِ ۚ وَلِلرِّجَالِ عَلَيْهِنَّ دَرَجَةٌ ۗ وَاللَّـهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ﴿٢٢٨
"Nao wake wana haki kama ambayo (waume zao) iliyo juu yao kwa mujibu wa Sharia; na wanaume wana daraja zaidi juu yao; na Allah ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Hakimu." [Al Baqarah 2:228]
Na Rasuli wa Allah صَليَ اللَّهُ علَيْهِ وَآله وسَلَّم amesema:
أَلَّا إِنَّ لَكُمْ عَلَى نِسَائِكُمْ حَقَا،ً وَلِنِسَائِكُمْ عَلَيْكُمْ حَقًا
"Tanabahini! Hakika nyinyi mnazo haki juu ya wanawake wenu, na wanawake wenu wanazo haki juu yenu..." tirmidhi, katika Kitabu cha kuhusu Kunyonyesha; mlango wa Yaliyokuja Kuhusu Haki za mwanamke juu ya mumewe; Hadithi namba (1163)
Na Rasuli wa Allah صَليَ اللَّهُ علَيْهِ وَآله وسَلَّم ameamuru kwamba haki za wake ziheshimiwe:
فَاتَّقُوا اللَّهَ فِي النِّسَاءِ فَإِنَّكُمْ أَخَذْتُمُوهُنَّ بِأَمَانِ اللَّهِ وَاسْتَحْلَلْتُمْ فُرُوجَهُنَّ بِكَلِمَةِ اللَّهِ
"...basi muogopeni Allah katika wake zenu! Kwani nyinyi mumewachukuwa kwa dhamana ya Allah, na mkahalalishiwa tupu zao kwa kalima ya Allah ...." Muslim, katika Kitabu cha Hajj; mlango wa Hija ya Nabii صَليَ اللَّهُ علَيْهِ وَآله وسَلَّم . Hadithi namba (1218a)
Hivyo basi kwa kadiri mume atakavyotimiza haki za mke wake, maisha yatakuwa ya haki, yenye furaha na kuridhika.
Haki za mke juu ya mumewe ni za aina mbili. حقوق الزوجة على الزوج قسمان
Ya Kwanza: Haki za kifedha حقوق مالية
Ya Pili: Haki zisizo za kifedha حقوق غير مالية
Haki zisizo za kifedha حقوق غير مالية
أعظم حقوق المرأة على زوجها المعاشرة بالمعروف والإحسان إليها
Haki kubwa zaidi ya mwanamke juu ya mumewe ni kukaa nae kwa wema na kumfanyia ihsani.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا يَحِلُّ لَكُمْ أَن تَرِثُوا النِّسَاءَ كَرْهًا ۖ وَلَا تَعْضُلُوهُنَّ لِتَذْهَبُوا بِبَعْضِ مَا آتَيْتُمُوهُنَّ إِلَّا أَن يَأْتِينَ بِفَاحِشَةٍ مُّبَيِّنَةٍ
﴾وَعَاشِرُوهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ ۚ فَإِن كَرِهْتُمُوهُنَّ فَعَسَىٰ أَن تَكْرَهُوا شَيْئًا وَيَجْعَلَ اللَّـهُ فِيهِ خَيْرًا كَثِيرًا ﴿١٩
"Enyi mlioamini! Si halali kwenu kuwarithi wanawake kwa kuwalazimisha, na wala msiwazuie kwa inda ili mpokonye baadhi ya vile mlivyowapa isipokuwa wakiwa wamefanya uchafu bayana; na kaeni nao kwa wema; na mkiwachukia, basi asaa mkachukia jambo na Allah Akalijaalia kuwa lenye heri nyingi ndani yake." [An Nisaa 4:19]