WAZEE WA FUMBA WAPINGA TATHMINI YA MAENEO YAO KWA AJILI YA UWEKEZAJI
ZANZIBAR YETU
0:00 / 0:00
WAZEE WA FUMBA WAPINGA TATHMINI YA MAENEO YAO KWA AJILI YA UWEKEZAJI
257 просмотров · 3 дн. назад
ZANZIBAR YETU
10,8 тыс. подписчиков
257 просмотров · 3 дн. назад
Wananchi wa Fumba wamesema wanahisi kana kwamba tayari wamekufa, lakini hawajazikwa, kutokana na kuchukuliwa kwa maeneo yao. Wamesema hawako tayari kupokonywa ardhi hiyo na kwamba bado wana malalamiko ambayo hayajapatiwa ufumbuzi.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mussa Thamir, maarufu kwa jina la Bozel, Mwanaidi Suleiman Haji na Mohammed Makame wamesema maeneo mengi yamechukuliwa, jambo linalowasikitisha. Wamedai kuwa tayari wameambiwa eneo la Kwale si lao tena, na sasa eneo la Fumba nalo linachukuliwa.
Bozel amesema kuwa wakati wa mlipuko wa COVID-19, vijana wengi walikosa kazi na baadhi yao wakaishia vituo vya polisi kutokana na tuhuma za wizi. Amewataka wenye mamlaka kuchukua hatua ili wananchi wasifikie hali hiyo na kukumbwa na hasara na madhara.
Kwa upande wake, Mwanaidi amesema wanaomba Rais wa Zanzibar mwenyewe azungumze na wananchi wa Fumba ili waelewe hatua za kuchukua. Amesema wanahofia kutumwa kwa watu kufanya tathmini pekee, bila wananchi kufahamishwa kinachokwenda kutathminiwa. Naye Mohammed Makame amesema kuwa kumekuwa na matukio yanayohusishwa na Mamlaka ya Uwekezaji, huku wananchi na ZIPA wakiwa bado hawajafahamiana.