Перейти к содержимому

MKUU WA WILAYA ATOA MASAA 24 WALIOSALIA NYATWALI KUONDOKA MARA MOJA

Mazingira Fm

0:00 / 0:00

MKUU WA WILAYA ATOA MASAA 24 WALIOSALIA NYATWALI KUONDOKA MARA MOJA

100 просмотров · 1 мес. назад
Mazingira Fm
2,77 тыс. подписчиков
100 просмотров · 1 мес. назад
Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Enock Kaminyoge, ametoa muda wa saa 24 kwa wananchi ambao bado wanaendelea kuishi katika eneo la Nyatwali, Wilaya ya Bunda, kuondoka katika eneo hilo ambalo kwa sasa ni eneo la hifadhi na linaweza kuhatarisha usalama wa maisha yao. Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 18, 2026, Kaminyoge Amesema Serikali iliamua kuongeza eneo la Hifadhi ya Taifa Serengeti mwaka 2022 kwa kutwaa eneo la Nyatwali lenye ukubwa wa ekari 14,250 lililokuwa ndani ya eneo la Bunda. Amesema Serikali ilifanya zoezi la uthamini wa mali za wananchi kwa mujibu wa sheria, ambapo jumla ya shilingi 53,407,045,111.87 ziliidhinishwa kwa ajili ya malipo ya fidia na zaidi ya wananchi 4,176 tayari wamelipwa fidia zao. Kaminyoge amesema takribani asilimia 95 ya wananchi waliolipwa fidia tayari wameondoka katika eneo hilo, huku takribani asilimia 5 wakiendelea kuishi katika eneo hilo licha ya maelekezo ya Serikali. Amesema wananchi hao wanapaswa kuondoka kwa kuwa Serikali tayari imeondoa huduma za kijamii katika eneo hilo, ikiwemo shule, vituo vya afya na miundombinu mingine ya Serikali, hali inayofanya kuendelea kuishi huko kuwa hatari na kukosa huduma muhimu. Aidha, Kaminyoge amesema wanyama kutoka Hifadhi ya Taifa Serengeti wameanza kusogea katika maeneo ya Nyatwali, hali ambayo inaweza kuongeza hatari kwa wananchi wanaoendelea kuishi katika eneo hilo. Ametaja wanyama hao kuwa ni pamoja na tembo, simba na fisi, ambao wanaweza kuhatarisha usalama wa binadamu. Kwa upande mwingine, Kaminyoge amesema eneo hilo pia limekuwa likitumiwa na baadhi ya watu wanaodaiwa kujihusisha na uhalifu kama sehemu ya kujificha baada ya kufanya uhalifu katika maeneo mbalimbali nchini. Hata hivyo, amesema Serikali haijapuuza madai ya wananchi ambao bado wana malalamiko kuhusu malipo ya fidia. Amesema baadhi ya maeneo na vikundi vya wananchi tayari vimewasilisha malalamiko yao serikalini na malalamiko hayo yanafanyiwa kazi, huku akieleza kuwa wananchi wenye madai yanayostahili kulipwa wataanza kupata fedha zao baada ya taratibu kukamilika. Mkuu huyo wa Wilaya amesema Serikali imekuwa ikitumia njia za mazungumzo, elimu na juhudi za kirafiki kuwawezesha wananchi kuhama, lakini baadhi yao wameendelea kubaki katika eneo hilo licha ya kufahamu kuwa kuendelea kuishi huko ni kinyume na utaratibu. Kwa msingi huo, Kaminyoge amesisitiza kuwa Serikali imetoa muda wa saa 24 kwa wananchi ambao bado wapo Nyatwali kuondoka katika eneo hilo, akieleza kuwa hatua hiyo inalenga zaidi kulinda usalama wa maisha ya wananchi pamoja na kuhakikisha eneo lililotengwa kwa ajili ya uhifadhi linatumika kwa madhumuni yaliyokusudiwa. #BUNDA #NYATWALI #youtubevideo