BI. MWENDAPOLE: WAZAZI WALEENI WATOTO WENU KIKAMILIFU, WALINDENI DHIDI YA UKATILI, AJIRA ZA UTOTONI
Nsimbo District Council
0:00 / 0:00
BI. MWENDAPOLE: WAZAZI WALEENI WATOTO WENU KIKAMILIFU, WALINDENI DHIDI YA UKATILI, AJIRA ZA UTOTONI
185 просмотров · 2 недели назад
Nsimbo District Council
11 подписчиков
185 просмотров · 2 недели назад
Divisheni ya afya kupitia sehemu ya ustawi wa jamii katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Agosti 27, imefanya ukaguzi, ufuatiliaji na usimamizi shirikishi wa masuala mbalimbali ya ustawi wa jamii kwa lengo la kutathmini hali ya ulinzi wa mtoto, usalama, na uzingatiaji wa sheria za ustawi wa jamii kwa kufuata miongozo hasa katika maeneo yenye vihatarishi vikubwa vya ustawi wa watoto na jamii kwa ujumla.
Bi. Theresia Mwendapole, ni Afisa Ustawi wa jamii kiongozi katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo akiambatana na maafisa wengie wa Ustawi wa jamii wametembelea baadhi ya maeneo huku wakianza ukaguzi katika vituo vya kulea watoto mchana yaani day care centers kwa lengo la kukagua ubora wa malezi, usalama wa mazingizra na uhalali wa uendeshaji wake ambapo vituo vitano vilikaguliwa.
Aidha, maafisa hao walifika katika maeneo ya machimbo ya madini yaliyoko Magula Kata ya Sitalike kufuatilia na kuzuia vitendo vya ajira za utotoni na uwepo wa watoto katika maeneo hatarishi.
Katika hatua nyingine maafisa hao pia walipita katika kumbi za kuonesha video kwa lengo la kuwatambua watoto waliotelekeza masomo na kujihusisha na michezo na burudani zisizostahili katika umri wao.
Bw. Mickson Stivin ni mwenyekiti wa Kitongoji cha Msasani kijiji cha Mtisi kata ya sitalike, yeye amewasihi wazazi na walezi kuwasimamia watoto wao .
Kufuatia ukaguzi huo, Bi Theresia Mwendapole amewasisitiza wazazi na walezi kutowaruhusu watoto wao kwenda machimboni, pamoja na Kumbi za kuonesha video na kushiriki katika michezo mbalimbali kinyume na sharia na sheria ya ulinzi wa mtoto.
Aidha, ametoa wito kwa wamiliki wa kumbi za video wanaokiuka sheria kufuata sheria, na taratibu za uendeshaji wake, huku akisisitiza kuwa oparesheni hizo zitakuwa endelevu ili kulinda mustakabali na usalama wa watoto na jamii kwa ujumla.