Перейти к содержимому

NYONYESHENI WATOTO KWA USAHIHI, TUWALINDE DHIDI YA UKATILI

Nsimbo District Council

0:00 / 0:00

NYONYESHENI WATOTO KWA USAHIHI, TUWALINDE DHIDI YA UKATILI

287 просмотров · 1 месяц назад
Nsimbo District Council
11 подписчиков
287 просмотров · 1 месяц назад
Wazazi wametakiwa kuwanyonyesha watoto kikamilifu ili kuijenga jamii yenye afya na kuondokana na changamoto za utapiamlo na udumavu katika jamii. Wito huo umetolewa leo na afisa lishe katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bi. Jackline Kitomari wakati akitoa elimu ya lishe kwa wakazi wa Kata ya Ibindi katika kilele cha wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama. Bi. Jackline amesema ni muhimu kuwanyoyesha watoto wachanga kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo ili kujenga kizazi bora kimwili na kiakili katika jamii pamoja na kuondoa changamoto za utapiamlo pamoja na udumavu katika jamii. Amesema kuwa unyonyeshaji hafifu wa maziwa ya mama unasababisha changamoto katika ukuaji wa watoto wachanga huku akitaja kitendo hicho kusababisha udumavu. “……… ni muhimu na ni lazima tunyonyeshe watoto ili tutengeneze kizazi ambacho kimekua kimwili lakini na kiakili ili tupunguze changamoto ya udumavu iliyopo……” Amesema Bi. Jackline Kitomari. Akisisitiza umuhimu wa wazazi wote wawili kushirkiana katika malezi ya watoto, Bw. Nickson Yohanes ambaye pia ni afisa lishe katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo amesema wazazi wa kiume wamekuwa wakikwepa majukumu yao katika malezi ya mtoto huku akitaja ushirikiano kuwa nguzo imara katika unyonyeshaji wa watoto wachanga, jambo linalojenga afya ya akili kwa watoto. Bwana Nickson amesema kuwa wanaume wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika mchakato wa unyonyeshaji sahihi wa watoto wachanga hasa kuhakikisha wanaepusha msongo wa mawazo kwa wake zao. Kwa upande wake, Bi. Mkami Makindi ambaye ni mratibu wa huduma za afya kwa baba mama na mtoto katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo amewasihi wazazi na walezi kuendelea kuwalinda watoto kwa nguvu zote dhidi ya ukatili unaoendelea kushamiri huku akitaja baadhi ya ukatili huo kufanywa na ndugu wa karibu wa watoto hao. Bi. Makindi amesema kuwa jamii inapaswa kuelewa kuwa malezi ya watoto siyo kuwapatia mahitaji yao pekee bali kuwalinda dhidi ya ukatili ili nao waweze kuwa kinara katika ulinzi dhidi ya ukatili kwa wenzao. “………… watoto wadogo wamekuwa wakifanyiwa matendo ya ukatili wa kijinsia ikiwepo kubakwa lakini pia na kulawitiwa……” Amesema Bi. Mkami. Katika Hatua nyingine Bi. Mkami amewaasa watoto kutokubali kushikwa sehemu yoyote ya miili yao kwani kuruhusu kufanya hivyo kunaweza kuwa mwanzo wa kufanyiwa ukatili dhidi yao. “………… kwahiyo watoto mnaonisikiliza, msikubaki mtu yeyote kukushika sehemu yoyote ya mwili wako, na imeonekana wengi wanaofanyiwa ukatili hufanywa na watu wa karibu, hivyo wito wangu kwa wazazi, msiruhusu watoto wenu walale na watu msiwafahau……….” Amesisitiza Bi. Mkami. Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo kupitia kitengo cha huduma za lishe imekuwa ikitoa elimu ya unyonyeshaji wa maziwa ya mama mara kwa mara katika jamii huku kilele cha wiki ya unyonyeshaj mwaka huu ikifanyika katika Kata ya Ibindi tarehe 8 Agosti ikiongozwa na kaulimbiu isemayo “mwanzo imara wa maisha ya mtoto huanza na maziwa ya mama”