Перейти к содержимому

WANANCHI CHAMWINO IKULU WAGOMEA FOMU ZA FIDIA YA ARDHI DC AINGILIA KATI.

CLOUDS HABARI

0:00 / 0:00

WANANCHI CHAMWINO IKULU WAGOMEA FOMU ZA FIDIA YA ARDHI DC AINGILIA KATI.

15 просмотров · 1 дн. назад
CLOUDS HABARI
2,26 тыс. подписчиков
15 просмотров · 1 дн. назад
WANANCHI CHAMWINO IKULU WAGOMEA FOMU ZA FIDIA YA ARDHI DC AINGILIA KATI. Takribani wananchi 2,000 wa vitongoji vya Maduma, Mpela na Mapinduzi katika kijiji cha Chamwino Ikulu, wilayani Chamwino mkoani Dodoma, wamegomea zoezi la upimaji wa ardhi katika maeneo yao, wakipinga utaratibu wa kutakiwa kusaini fomu za kukubali fidia badala ya fomu za utambuzi wa maeneo yao. Wananchi hao wamesema utaratibu huo umewafanya kusitisha zoezi hilo kwa madai kuwa hawapo tayari kusaini nyaraka zinazohusisha masuala ya fidia kabla ya kupata ufafanuzi wa kina kuhusu maana na athari zake. Wakizungumza mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Chamwino,Janeth Mayanja, aliyefika katika eneo hilo kutatua mgogoro huo, wananchi wameeleza kutoridhishwa na utaratibu uliowekwa, wakisisitiza kuwa wanahitaji fomu za utambuzi wa maeneo yao badala ya nyaraka za kukubali fidia Hata hivyo, baada ya kusikiliza malalamiko ya wananchi na maelezo ya viongozi wa halmashauri, Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Janeth Mayanja, amefuta zoezi hilo na kuagiza lianze upya ili wananchi wapate ufafanuzi na utaratibu unaoeleweka kabla ya kuendelea na hatua za upimaji. Uamuzi huo unafungua ukurasa mpya wa utekelezaji wa zoezi la upimaji na urasimishaji wa ardhi katika vitongoji hivyo, huku wananchi wakisubiri kuanza upya kwa zoezi hilo kwa utaratibu utakaozingatia uelewa na ushiriki wao. @jamesbunuma #cloudsdigitalupdates