Перейти к содержимому

SIMULIZI YA MWANAFUNZI ALIYETOROSWA KWA NGUVU MOROGORO / SIMULIZI YA ALIYETOROSHWA KUOLEWA KWA NGUVU

CLOUDS HABARI

0:00 / 0:00

SIMULIZI YA MWANAFUNZI ALIYETOROSWA KWA NGUVU MOROGORO / SIMULIZI YA ALIYETOROSHWA KUOLEWA KWA NGUVU

27 просмотров · 1 дн. назад
CLOUDS HABARI
2,26 тыс. подписчиков
27 просмотров · 1 дн. назад
SIMULIZI YA ALIYETOROSHWA KUOLEWA KWA NGUVU Mwanafunzi aliyechukuliwa kwa nguvu na vijana wanne akitokea shuleni akiwa na wenzake wakati wakisubiri usafiri wa kurudi nyumbani ameeleza namna tukio hilo lilivyokuwa. Akizungumza na Clouds Digital, Mwanafunzi huyo amesimulia kuwa tukio hilo limetokea wakati akitoka kujaza taarifa za machaguo ya kidato cha tano na vyuo katika Shule ya Sekondari Sokoine Memorial wilayani Mvomero, ambapo baada ya kuchukuliwa akapelekwa kuhifadhiwa katika nyumba ambayo hakuruhusiwa kutoka nje na hadi sasa hajui alipelekwa eneo gani licha ya tiketi yake aliyopewa akiwa ndani ya basi alilotumia kurudi nyumbani ilisomeka katokea Kibaigwa wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma. Aidha amesema akiwa katika nyumba aliyohifadhiwa alikuwa akishawishiwa pia kuolewa kwasababu ni suala la kimila huku akiomba jamii za wafugaji kuachana na vitendo vya kukatisha ndoto za wasichana wa jamii hiyo.