Перейти к содержимому

MKUU WA MAJESHI Jenerali Venance Mabeyo Azindua Kituo cha Burudani cha JKT Jijini Dodoma

Ulinzi Channel

0:00 / 0:00

MKUU WA MAJESHI Jenerali Venance Mabeyo Azindua Kituo cha Burudani cha JKT Jijini Dodoma

29 635 просмотров · 4 года назад
Ulinzi Channel
87,3 тыс. подписчиков
29 635 просмотров · 4 года назад
JKT YAZINDUA ENEO LA BURUDANI JIJINI DODOMA Jeshi la Kujenga Taifa chini ya Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele limezindua eneo la Burudani katikati ya Jiji la Dodoma maeneo ya Medeli East Eneo hilo lenye mvuto wa Kiburudani limezinduliwa tarehe 29 Oktoba 2021 na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Salvatori Mabeyo ambapo Mradi huo utahusisha Ukumbi Mkubwa wa Meja Jenerali Rajabu Manele "MABELE HALL" Ukumbi huo una uwezo wa kuchukua watu 1000 hadi 1200, Ukumbi mdogo, Jengo la Utawala, VIP Lounge na Ujenzi wa eneo la michezo ya Watoto. Akiuelezea Mradi huo mbele ya mgeni rasmi, Mkuu wa Utawala JKT Brigedia Jenerali Hassan Mabena, alieleza kuwa upatikanaji wa eneo hilo ulitokana na juhudi za aliyekuwa Kamanda Kikosi wa 834 Makutupora JKT Kanali Menas Thomas Mbele (Mstaafu) ambaye alihakikisha analinunua eneo hilo kwa manufaa ya Jeshi licha ya changamoto ya uhaba wa raslimali fedha iliyokuwa inakikabili kikosi hicho. Naye Kanali Menas Thomas Mbele (Mstaafu) alikuwa ni miongoni mwa wageni waalikwa kwenye uzinduzi huo ikiwa ni Kutambua mchango wake wa Kizalendo na kuipenda Nchi yake ambapo alitoa Rai kwa Makamanda na viongozi Wengine kuiga mfano wake kutanguliza maslahi mapana ya Taifa badala ya kujinufaisha mtu mmoja mmoja, “Pale Makutupora tulinunua Trekta na Gari (Lori) kwa hela ya Mchicha, nilipohama kwenda Ruvu JKT nialiacha Ng’ombe 100” alieleza Kanali MBele (Mstaafu). Akiongea kabla ya kumkaribisa Mkuu wa Majeshi, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Rajabu Mabele alimweleza Mgeni rasmi kuwa uanzishwaji wa Mradi huo ni kuitikia wito na maelekezo ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Salvatory Mabeyo ya kuvitaka vikosi na taasisi chini ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kwa Kuanzisha miradi ya Kitega Uchumi ili kupunguza changamoto inayotokanana na Nakisi ya Bajeti ya Serikali kwa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Akizungumza kabla ya Uzinduzi wa eneo la Burudani la JKT, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Salvatory Mabey alimpongeza Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele kwa Ubunfu wa kuanzisha miradi mikubwa kama hio, hii ni pamoja na watangulizi wake wote waliowahi kuliongoza JKT Aidha, amewataka viongozi watakaousimamia mradi huo ulipo Medeli East Jijini Dodoma kuwa wabunifu na kuziboresha huduma zao kuwa za kiushindani ili kuvutia Maafisa, Askari na wanachi wa Jiji la Dodoma kupafanya sehemu ya Buruani kweli kweli. Akihitimisha Hotuba yake, Mkuu wa Majeshi aliwakumbusha JKT kuongeza kasi katika uzalishaji mali hasa Kilimo ili kufikia azma ya Serikali ya kufiki 2025 Jeshi la Kujenga Taifa lianze kujilisha badala ya kutegemea Bajeti kuu ya Serikali.