TAZAMA ASKOFU MALASUSA ALIVYOZINDUA JENGO LA BIL.6.5 HAYDOM # NCHI KAMA HIZO MSIACHE KUZIOMBEA
Bibititi Tv
0:00 / 0:00
TAZAMA ASKOFU MALASUSA ALIVYOZINDUA JENGO LA BIL.6.5 HAYDOM # NCHI KAMA HIZO MSIACHE KUZIOMBEA
207 просмотров · 1 год назад
Bibititi Tv
2,95 тыс. подписчиков
207 просмотров · 1 год назад
FURAHA YA KUISHI MBINGUNI NI LAZIMA IANZIE HAPA DUNIANI
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania ( KKKT) Askofu Dkt. Alex Malasusa amezindua jengo la Mama na mtoto la Hospitali ya Rufaa ya Kilutheri ya Haydom wilayani Mbulu Mkoani Manyara, lenye thamani ya sh.bil.6.5 kwenye jubilei ya miaka 70 ya Hospitali hiyo.
Akizungumza hizi karibuni kwenye Maadhimisho ya miaka 70 ya jubilee ya Hospitali hiyo Dkt. Malasusa amesema Hospitali hiyo Ina mchango mkubwa sana katika kulihudumia Taifa la Tanzania kwani jumla ya wilaya 7 na mikoa 4 wananchi wake wanapatiwa huduma katika hospitali hiyo tena Kwa kupatiwa huduma iliyo Bora kabisa.
Askofu Malasusa amesema Wamiaionanari walipofika Haydom walipelekq habari njema ya uwokovu na kuwasukuma kuanzishwa Hospitali hiyo iliyoanzishwa Mwaka 1955.
" Hospitali yetu hii ya haydomimeendelea na kuboresha miundombinu yake kwa kujenga jengo la Mama na mtoto kubwa na la kisasa lililogharimu jumla ya sh.Bil. 6.5, ni hilo mnaloliona hapo pembeni yetu Kwa mliochelewa wakati wa uzinduzi, nimelizundua hii Leo" amesema Askofu Dkt. Malasusa.
Aidha amesema Wamisionari walipopeleka wokovu Haydom wilayani Mbulu Mkoani Manyara ni kwa sababu ya wokovu ambalo ni jambo la Mbinguni tu, hivyo wametakiwa kutambua kuwa furaha ya kwenda Mbinguni lazima ianzie na hapa Duniani na si vinginevyo.