UKUAJI WA KIROHO (Sehemu ya IX) - Pastor Robert Mwaisaka
Pastor Robert Mwaisaka
0:00 / 0:00
UKUAJI WA KIROHO (Sehemu ya IX) - Pastor Robert Mwaisaka
18 просмотров · 3 нед. назад
Pastor Robert Mwaisaka
90 подписчиков
18 просмотров · 3 нед. назад
Mtu pekee anayekidhi vigezo vya kufundisha kuhusu Mungu ni Yesu. Mwamini anapaswa kujikita katika hili yaani kumruhusu Yesu kuwa chanzo sahihi cha taarifa kuhusu Mungu. Hakuna malaika anayeruhusiwa kumfundisha mwamini. Kila jaribio la kutaka kufundishwa na Malaika linapelekea Upotevu. Malaika wanapaswa kufundishwa na kuongozwa na waamini.
Waefeso 3:8 Mimi, niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo wa watakatifu wote, nalipewa neema hii ya kuwahubiri Mataifa utajiri wake Kristo usiopimika; 9 na kuwaangaza watu wote wajue habari za madaraka ya siri hiyo, ambayo tangu zamani zote ilisitirika katika Mungu aliyeviumba vitu vyote; 10 ili sasa, kwa njia ya kanisa, hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ijulikane na falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho;
Kanisa ndiyo mwalimu wa Malaika. Kama Malaika watataka kumjua Mungu, wanapaswa wajifunze kwa waamini, kwani ufunuo wa Mungu ulitolewa kwa waamini na sio malaika.