SALAMU ZA SHUKRANI KIZIMKAZI KUTOKA TIRA
Tanzania Insurance Regulatory Authority [TIRA]
0:00 / 0:00
SALAMU ZA SHUKRANI KIZIMKAZI KUTOKA TIRA
405 просмотров · 1 месяц назад
Tanzania Insurance Regulatory Authority [TIRA]
260 подписчиков
405 просмотров · 1 месяц назад
Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) inatoa shukrani za dhati kwa wananchi wa Kizimkazi kwa mapokezi mazuri, ushirikiano na ushiriki wao katika kuendelea kuelimisha jamii kuhusu umuhimu na faida za bima.
TIRA inawapongeza wananchi wa Kizimkazi kwa kuunga mkono jitihada za kuongeza uelewa wa bima na kuhimiza matumizi ya huduma za bima kama sehemu muhimu ya kujikinga dhidi ya majanga na kulinda maisha, mali na shughuli za kiuchumi.
Tunaamini kuwa kupitia ushirikiano wa karibu kati ya TIRA, wadau wa sekta ya bima na wananchi, tunaweza kujenga jamii yenye uelewa mpana wa bima, ulinzi madhubuti na ustahimilivu wa kiuchumi.
Asanteni sana Kizimkazi kwa mapokezi na ushirikiano wenu. ❤️
📌 Endelea kutufuatilia kwa taarifa, elimu na habari mbalimbali kuhusu sekta ya bima nchini.