Перейти к содержимому

ASKOFU DKT. MSAFIRI MBILU AWATAKA WAZAZI KUWALEA WATOTO KATIKA MAADILI MEMA.

KKKT DKMS Online TV

0:00 / 0:00

ASKOFU DKT. MSAFIRI MBILU AWATAKA WAZAZI KUWALEA WATOTO KATIKA MAADILI MEMA.

109 просмотров · 5 дней назад
KKKT DKMS Online TV
9,48 тыс. подписчиков
109 просмотров · 5 дней назад
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, amewataka wazazi kutambua wajibu wao wa kulea watoto katika maadili mema na mafundisho ya Kikristo, akisisitiza kuwa malezi ya watoto ni jukumu la familia, kanisa na jamii kwa ujumla. Askofu Mbilu amesema hayo leo katika ibada ya Jumapili ya siku ya Bwana ya 17 baada ya Utatu iliyofanyika katika, KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Usharika wa Magamba, wakati wa mahubiri ambapo amesema watoto wanapaswa kuwatii wazazi wao katika Bwana na kuwaheshimu , huku wazazi nao wakitakiwa kutowachokoza watoto, bali kuwalea katika adabu na maonyo ya Bwana. Amesema mtoto anapozaliwa si mali ya familia pekee, bali ni sehemu ya jamii, hivyo jamii nzima, pamoja na kanisa, ina wajibu wa kushiriki katika malezi na ustawi wa watoto. Askofu Mbilu pia amesisitiza kuwa watoto wanapaswa kuwatii wazazi wao katika mambo mema yanayolingana na mapenzi ya Mungu, akieleza kuwa kumtii mzazi katika mambo mema ni sehemu ya kujifunza kumtii Mungu. Kwaupande wa washarika waliohudhuria katika Ibada hiyo Peter Jali,Mwivei Kusaga na Mwinjilisti Fikirini Chando wamesema mahubiri ya siku ya leo yameendana na siku hii ya mikaeli na watoto. Katika Ibada hii iliyofanyika katika usharika huu wa Magamba unaoongozwa na Mchungaji Salome Hizza Walalaze jumla ya Vijana 55 wa kipaimara wamebarikiwa na wawili kati yao kubatizwa