Перейти к содержимому

Wananchi Kata ya Mkundi waiomba Serikali.

RS MOROGORO

0:00 / 0:00

Wananchi Kata ya Mkundi waiomba Serikali.

453 просмотра · 5 лет назад
RS MOROGORO
2,23 тыс. подписчиков
453 просмотра · 5 лет назад
Wananchi wa Kata ya Mkundi wameiomba serikali kuwajengea miundombinu ya Shule ya Msingi ya Mkundi iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ili kuwaondolea adha wanazokumbana nazo wanafunzi Shuleni hapo. Ombi hilo limetolewa leo Februari 16 mwaka huu mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare alipotembelea Shuleni hapo kwa ajili ya kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa na kuona changamoto mbalimbali zinazoikuba shule hiyo. Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi wa Kata hiyo akiwemo Bi. Khadija Ramadhani amesema shule hiyo inakabiliwa na uchache wa vyumba vya madarasa hali ambayo inapelekea wanafunzi hao kubanana katika darasa moja. Naye Ayoub Nzezela Mkazi wa Kata ya Mkundi amebainisha kuwa baadhi ya wanafunzi katika Shule hiyo wanakaa chini kutokana na upungufu wa madawati licha ya jitihada kubwa ambazo amezifanya za ukarabati wa madawati shuleni hapo. Akizungumza na wananchi wa Kata hiyo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare amesema changamoto zilizopo katika shule hiyo zinasababishwa na wazazi kwa kiasi fulani kutokana na kushindwa kuonesha ushirikiano katika kujenga miundombinu ya Shule hiyo. Loata Sanare amebainisha kuwa licha ya changamoto nyingi zilizopo katika shule hiyo walimu wa shule hiyo wameshindwa kuwa wabunifu kutokana na pesa ambayo Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro alizileta shuleni hapo kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa. Aidha, Loata Sanare amewataka walimu, bodi ya Shule na viongozi wa kata kuitisha kikao cha wazazi ili kuangalia namna ya kutengeneza miundombinu ya shule hiyo kisha kupeleka mrejesho wa kikao hicho kwa Mkuu wa Wilaya kwa ajili ya kutoa kibali cha kuchangia ujenzi wa Shule hiyo. ‘’Lazima tufanye kitu hapa lakini tuwashirikishe na wazazi, itisha kikao cha wazazi waje kushuhudia namna ambavyo watoto wao wanasoma, wazazi watatwambia kutokana na hali hii sasa tufanye nini, chukua hayo maamuzi yaliyotoka kwa wazazi andikia muhtasari mpelekee Mkuu wa Wilaya, hayo ndiyo yatakuwa maamuzi ya wazazi wa watoto wa shule hii’’ amesema Sanare Sambamba na hayo, Loata Sanare amewataka watendaji wa kata kuwahimiza wananchi wa Kata hiyo kushiriki katika ujenzi wa barabara itayojengwa kwa nguvu za wananchi kuelekea shule hiyo ya msingi Mkundi ambapo TARURA itamalizia pale ambapo wananchi watakapoishia.