MGAWANYO WA ARDHI: AINA TATU ZA ARDHI NCHINI TANZANIA
MEVITY COMPANY LTD
0:00 / 0:00
MGAWANYO WA ARDHI: AINA TATU ZA ARDHI NCHINI TANZANIA
129 просмотров · 9 дней назад
MEVITY COMPANY LTD
791 подписчик
129 просмотров · 9 дней назад
MGAWANYO WA ARIDHI NCHINI TANZANIA:-
Nchini Tanzania Aridhi imegawanywa kwenye makundi 3 yafuatayo;-
1. Aridhi ya Jumla( General Land)
Ni Aridhi inayojumuisha Halmashauri za Majiji, Manispaa, Miji na Miji midogo na Maeneo karibu na Miji.
Aridhi KUU ndio huwa inapangwa kuwa na Makazi na Uwekezaji mbalimbali kwenye Miji na Maeneo yote ya Halmashauri husika.
2. ARIDHI ILIYOHIFADHIWA ( Reserved Land)
Aridhi iliyohifadhiwa imeganyika sehemu kuu tatu;-
A. Aridhi ya Hifadhi za Wanyama na Misitu
Aridhi hii imetengwa kwa Ajili ya Wanyama pori, Misitu na Uoto wa Asili.
B. Aridhi ya JESHI.
Aridhi hii imetengwa kwa Ajili ya Jeshi la Wananchi, Jeshi la Kujenga Taifa, Jeshi la Polisi n.k. kwa shughuli zao.
C.Aridhi ya Serikali ( Government Land Bank)
Aridhi hii imetengwa kwa Ajili ya Matumizi ya miaka Ijayo ( baadae)kwa Serikali.
3. ARIDHI YA VIJIJI ( Village Land)
Aridhi hii imetengwa kwa Vijiji na ipo chini ya Hati za Kimila (Customary Law).
Kila kijiji kina Ukubwa tofauti tofauti wa Aridhi kulingana na Vigezo tofauti kabla na baada ya Ukoloni. Vijiji vingi vilianzishwa kipindi Cha Ujamaa na Kujitegemea chini ya Baba wa Taifa, Mwl. Julius K. Nyerere.
NB: Ardhi za Maeneo ya Makaburi, MIUNDOMBINU kama Barabara &Nguzo za Umeme, Vyanzo vya Maji, Sehemu za Kuhifadhi Taka n.k. zinajumuishwa kwenye kundi la ARDHI iliyohifadhiwa.
HITIMISHO: Tanzania bado Ina Ardhi kubwa Kwa Kilimo, Makazi na Shughuli zingine ukilinganisha na Mataifa Jirani.
Kwa Maeneo ya Mijini Ushindani wa kumiliki Ardhi ni Mkubwa.