Перейти к содержимому

MAGALAMBULA AMUOMBA HECHE AMTAKE RADHI MBOWE

TANZANITE TV

0:00 / 0:00

MAGALAMBULA AMUOMBA HECHE AMTAKE RADHI MBOWE

2 290 просмотров · 13 ч назад
TANZANITE TV
293 тыс. подписчиков
2 290 просмотров · 13 ч назад
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee CHADEMA Kanda ya Kati na mwanachama mwanzilishi wa chama, Acquilin Magalambula, amemkosoa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche, kwa kauli anazodai zinamlenga kumshusha hadhi aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe. Magalambula amesema Heche anapaswa kutumia nafasi yake kuzungumza na Mbowe moja kwa moja endapo kuna jambo analoliona haliko sawa, badala ya kulizungumzia kwenye mikutano ya hadhara. Amesema Mbowe ana nafasi ya kuwa mjumbe wa Kamati Kuu kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA, hivyo kuna umuhimu wa viongozi kuheshimiana na kujenga mshikamano ndani ya chama. Magalambula amemtaka Heche kumuomba radhi Mbowe, huku akizitaka mamlaka za chama kumuita na kumchukulia hatua za kinidhamu endapo ataendelea kumzungumzia hadharani kwa namna hiyo. Amesema viongozi wanapaswa kuelekeza nguvu katika kujenga sera na kuwashawishi wananchi kukiunga mkono CHADEMA.