WAZIRI KITWANA AKABIDHIWA MAGARI NA WIZARA YA FEDHA
OFISI YA RAIS TAMISEMIM ZANZIBAR
0:00 / 0:00
WAZIRI KITWANA AKABIDHIWA MAGARI NA WIZARA YA FEDHA
1 397 просмотров · 11 дн. назад
OFISI YA RAIS TAMISEMIM ZANZIBAR
3,92 тыс. подписчиков
1 397 просмотров · 11 дн. назад
Waziri wa fedha na mipango zanzibar mh. Juma malik akili amesema mradi wa big-z unalenga kusaidia kuboresha miundombinu mbalimbali ikiwemo barabara na masoko pamoja na kuimarisha huduma za usafi hatua inayolenga kuleta haiba nzuri ya miji.
Ameyasema hayo katika hafla ya makabidhiano ya magari ya usafi kati ya wizara ya fedha na mipango na ofisi ya rais tawala za mikoa serikali za mitaa na idara maalum za smz iliyofanyika katika ukumbi wa wizara fedha na mipango zanzibar.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa magari hayo waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za mikoa serikali za mitaa na idara maalum za smz mheshimiwa idrissa kitwana mustafa ameishukuru wizara ya fedha na mipango na kuahidi kuwa magari hayo yatakabidhiwa katika maeneo husika na kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa.
Aidha mh. Idrissa amesema matumizi sahihi ya magari hayo yatasaidia kuimarisha huduma za usafi katika manispaa za zanzibar na hivyo kuchangia katika juhudi za serikali za kuhakikisha mazingira ya zanzibar yanakuwa safi na salama.
Kwa upande wake kaimu katibu wa wizara ya fedha na mipango zanzibar nd aboud hassan mwinyi amesema mradi huo unahusisha ununuzi wa magari ya ukusanyaji taka ujenzi wa vizimba pamoja na ujenzi wa vituo vya kuhamishia taka. Pia mchakato wa ununuzi wa magari umekamilika huku wizara ikiwa tayari imesaini mkataba kwa ajili ya ujenzi wa vizimba na hatua nyingine za utekelezaji wa mradi zikiendelea.
Jumla ya magari 26 yamekabidhiwa kwa ofisi ya rais tawala za mikoa serikali za mitaa na idara maalum za smz ambapo magari 15 ni tipa na magari 11 ni compactors magari hayo yanatarajiwa kutumika katika manispaa za zanzibar kwa ajili ya ukusanyaji na usafirishaji wa taka ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa juhudi za serikali katika kuboresha usafi wa mazingira na afya ya jamii