VIKOSI VYA ULINZI NA USALAMA ZANZIBAR VYA PATIWA MAFUNZO KUELEKEA AFCON 2027
OFISI YA RAIS TAMISEMIM ZANZIBAR
0:00 / 0:00
VIKOSI VYA ULINZI NA USALAMA ZANZIBAR VYA PATIWA MAFUNZO KUELEKEA AFCON 2027
2 246 просмотров · 3 нед. назад
OFISI YA RAIS TAMISEMIM ZANZIBAR
3,92 тыс. подписчиков
2 246 просмотров · 3 нед. назад
MKOA WA MJINI /MAGH VIKOSI VYA ULINZI NA USALAM ZANZIBAR VYAPATIWA MAFUNZO KUELEKEA YA AFCON 2027 27/08/2026
Ndugu Issa Mahfoudh Haji Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ amevitaka vikosi vya ulinzi na usalama kuzingatia mafunzo watakayopatiwa ili kuhakikisha mashindano ya Afcon 2027 yanafanyika kwa amani visiwani Zanzibar .
Ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa vikosi vya ulinzi na usalama yaliyofanyika katika ukumbi wa Jaji Mstaafu Hamid Mahmoud Maisara Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kwa lengo la kuwajengea uwezo maafisa hao.
Amesema ulinzi utahitajika katika viwanja wakati wa mechi, maeneo ya viwanja vya mazoezi, hotelini pamoja na maeneo ya vivutio vya watalii yatakayotumiwa na wageni kutoka mataifa mbalimbali, hivyo ipo haja ya kuyatumia vyema mafunzo muda utakapofika.
Kwa upande wake katibu mtendaji baraza la michezo Said Marin amesema Zanzibar ipo tayari kwa mashindano baada ya kufanyiwa ukaguzi wa miundombinu inayohusiana na mpira wa miguu, huku akisisitiza umuhimu wa usalama katika mashindano hayo.
Nao wakufunzi wa mafunzo hayo Ramadhan Abdalla Bakar Mkuu wa ulinzi na usalama wa chama cha mpira Zanzibar Zff na Mrakibu wa Jeshi la Polisi Mohammed Manyahe kutoka Dar Es Salaamwamesema mafunzo hayo yatawasaidia wadau wa ulinzi kwa kupunguza hatari na kujua namna ya kuchukua hatua wakati wa dharura.
Kwa upande wao waliopatiwa mafunzo hayo wamesema watayatumia vyema mafunzo waliyopatiwa ili kuipatia sifa nzuri Zanzibar na Tanzania kwa ujumla ambapo mashindano hayo ya Afcon yanatarajiwa kufanyika mwakani kwa nchi ya Tanzania,Uganda na Kenya.