Перейти к содержимому

FORODHANI YANG’ARA TENA, MEYA KAMAL AONGOZA ZOEZI LA USAFI

ASAM Online TV

0:00 / 0:00

FORODHANI YANG’ARA TENA, MEYA KAMAL AONGOZA ZOEZI LA USAFI

1 795 просмотров · 3 дн. назад
ASAM Online TV
22,1 тыс. подписчиков
1 795 просмотров · 3 дн. назад
Mapema leo, upepo mwanana wa bahari katika Bustani ya Forodhani uliambatana na sauti za mafagio na mikono ya pamoja ikisafisha kila pembe ya eneo hilo maarufu la kihistoria na utalii Zanzibar. Mstahiki Meya wa Jiji la Zanzibar, Mhe. Kamal Haji, ameongoza zoezi la usafi katika Bustani ya Forodhani, akieleza kuwa kutunza eneo hilo ni wajibu wa kila mwananchi ili kulifanya Jiji la Zanzibar kuwa na mwonekano mzuri kwa wakazi na wageni. Akifafanua mkakati wa kuhakikisha usafi unaendelea, Mkuu wa Divisheni ya Huduma za Jamii, Miundombinu na Mambo Mtambuka ambaye pia ni Msimamizi Mkuu wa Bustani ya Forodhani, Mwalimu Ali, amesema usimamizi wa maeneo ya wazi utafanyika kila siku. Amesema miundombinu yote ya usafi itasimamiwa kwa karibu ili kuhakikisha Bustani ya Forodhani inaendelea kubaki katika hali ya usafi na muonekano unaoridhisha muda wote. Kwa upande wa wadau wa maendeleo, Joseph Singano kutoka Shirika la Otesha, amesema wataendelea kushirikiana na Mamlaka ya Jiji katika kuboresha uoto wa asili na kutunza mazingira, hatua inayolenga kuifanya Forodhani kuwa mfano wa kuigwa katika utunzaji wa mazingira ya jiji. #AsamOnlineTV #Forodhani #Zanzibar #KamalHaji #JijiLaZanzibar #Usafi #Mazingira #Utalii #ZanzibarTourism #Otesha #GreenZanzibar #Habari #ZanzibarNews #Tanzania #TikTokTanzania #InstagramTanzania #Trending #FYP #ForYou #Viral