Перейти к содержимому

MTUHUMIWA WA UHALIFU APIGWA RISASI KILOSA

ITV Tanzania

0:00 / 0:00

MTUHUMIWA WA UHALIFU APIGWA RISASI KILOSA

409 просмотров · 14 часов назад
ITV Tanzania
1,37 млн подписчиков
409 просмотров · 14 часов назад
‎ ‎#HABARI: Mtu mmoja anayetuhumiwa kwa matukio ya mauaji, ubakaji na wizi wa kutumia silaha, Nanei Kokan State (30), mkazi wa Kijiji cha Parakuyo wilayani Kilosa mkoani Morogoro, amefariki dunia baada ya kupigwa risasi na askari polisi waliofika kumkamata. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, ACP Andrew Kantimbo, ameeleza kuwa mtuhumiwa huyo alijifungia chumbani huku akiwateka mwanamke na mwanaye mdogo kama ngao na kutishia kuwaua kwa sime iwapo polisi wangemsongelea, hatua iliyowalazimu maofisa wa jeshi hilo kuchukua hatua hiyo ili kuokoa maisha ya mateka. Baba mzazi wa marehemu amekiri mwanaye kujihusisha na matukio ya kiuhalifu mara kwa mara licha ya kujaribu kumkanya, huku Mwenyekiti wa Kijiji cha Parakuyo, Emmanuel Kibasisi, akiwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa serikali ili kutokomeza uhalifu. Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limeendelea kuwasihi vijana kujiepusha na vitendo vya kiuhalifu na badala yake kujishughulisha na kazi halali za kujipatia kipato, pamoja na kuomba wadau kuongeza juhudi za kutoa elimu ya malezi bora katika jamii. ‎ Powered by #MCHEZOSUPA ‎ ‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA: ‎- ‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M - Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV. ‎ ‎#ITVDigital #ITVUpdates ITVTanzania ‎Follow @itvtz @radioonetanzania ‎@capitaldigitaltanzania