Перейти к содержимому

MSIGWA MUONGO, AMELETA TAARIFA NYINGI ZA CHADEMA, NASHANGAA KAMA WATAMWAMINI TENA

ALU TV

0:00 / 0:00

MSIGWA MUONGO, AMELETA TAARIFA NYINGI ZA CHADEMA, NASHANGAA KAMA WATAMWAMINI TENA

897 просмотров · 1 день назад
ALU TV
11 тыс. подписчиков
897 просмотров · 1 день назад
Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Kenani Kihongosi, amemkosoa Msigwa akidai kuwa alijiunga na Chama cha Mapinduzi baada ya kukosa uongozi ndani ya CHADEMA, huku akieleza kuwa CCM ni chama kinachopokea wanachama kutoka makundi mbalimbali. Kihongosi amesema CCM ilimfungulia milango Msigwa na kumpokea kama mwanachama, akieleza kuwa chama hicho kinaamini katika usawa wa binadamu na haki sawa kwa wanachama wake. Amedai kuwa baada ya kujiunga na CCM, Msigwa alizunguka maeneo mbalimbali nchini akieleza mambo mabaya kuhusu CHADEMA, lakini baadaye akaanza kuomba nafasi za uongozi ndani ya CCM. Kwa mujibu wa Kihongosi, Msigwa alitaka kupewa nafasi ya ukuu wa mkoa, ukuu wa wilaya au uwaziri, lakini CCM ilieleza kuwa ina utaratibu wake wa kuchagua viongozi na hazina kubwa ya makada wanaostahili nafasi hizo. Kihongosi amedai kuwa baada ya kutopata nafasi alizokuwa akizihitaji, Msigwa alianza kuikosoa CCM. Amesema ana taarifa kuhusu mwenendo wake na kwamba wakati ukifika ataweka wazi ushahidi anaodai kuwa anao.#alutv #alutvupdates