Перейти к содержимому

Lissu kususia chakula kudai haki yake ya faragha

DW Kiswahili

0:00 / 0:00

Lissu kususia chakula kudai haki yake ya faragha

1 288 просмотров · 2 дн. назад
DW Kiswahili
337 тыс. подписчиков
1 288 просмотров · 2 дн. назад
Mwanasheria Mkuu wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, CHADEMA, Rugemeleza Nshala, amesema Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu, anayeshikiliwa gerezani, anatarajia kuanza mgomo wa kula kuanzia Jumatatu, Oktoba 26, hadi pale atakapopewa haki ya kukutana na mawakili wake kwa faragha. Nshala amesema Lissu amepinga utaratibu wa mazungumzo yake na mawakili kufanyika mbele ya maafisa wa magereza, akisisitiza kuwa hali hiyo inakiuka haki. Ameeleza kuwa tayari Mahakama Kuu ya Tanzania ilishatoa uamuzi unaozuia mawasiliano kati ya Lissu na mawakili wake kusikilizwa au kufuatiliwa. Kwa mujibu wa wakili huyo, hatua ya mgomo wa kula inalenga kushinikiza utekelezaji wa haki hiyo ya msingi ya kisheria hadi madai yake yatakapopatiwa ufumbuzi.