EXCLUSIVE INTERVIEW WITH FOOTBALLER JUMA SHABANI (ANKO J) | HOSTED BY PAUL OJ
80s Vibe Media
0:00 / 0:00
EXCLUSIVE INTERVIEW WITH FOOTBALLER JUMA SHABANI (ANKO J) | HOSTED BY PAUL OJ
2 404 просмотра · 7 месяцев назад
80s Vibe Media
6,35 тыс. подписчиков
2 404 просмотра · 7 месяцев назад
Katika interview hii, mtangazaji Mr Paul OJ amekaa chini na mchezaji wa zamani wa Yanga SC, Pan Africa pamoja na Timu ya Taifa (Taifa Stars), anayefahamika kama Juma Shabani maarufu kama Anko J.
Anko J amefunguka kwa undani kuhusu maisha ya soka katika enzi zao, changamoto walizopitia wachezaji wa zamani, na tofauti kubwa kati ya soka la zamani na la sasa. Pia amezungumzia wachezaji wakubwa aliowahi kucheza nao, pamoja na michezo migumu zaidi iliyowahi kumpa presha kubwa katika maisha yake ya soka.
Mbali na hilo, Anko J ametoa ushauri mzito kwa vijana wanaopenda au wanaocheza mpira wa miguu, akisisitiza nidhamu, uvumilivu na mapenzi ya kweli kwa mchezo. Katika mahojiano haya pia hakusita kutoa ushauri kwa viongozi wa mpira wa miguu Tanzania, hususan Rais wa Yanga SC, Eng. Hersi Said, akimpongeza kwa uongozi wake bora na namna anavyoendesha klabu ya Yanga kitaalamu.
Karibu kutazama.
#AnkoJ #JumaShabani #MrPaulOJ #YangaSC #TaifaStars #SokaTanzania #HistoriaYaSoka #PanAfrica #EngHersiSaid